Saturday 23 August 2014

BADO KUNACHANGAMOTO KATIKA UCHANGIAJI DAMU KWA NYANDA ZA JUU KUISINI



 Afisa uhamasishaji wa nyanda za juu kusini Charton Meena


KATIKA kukabiliana na changamoto ya uchangiaji damu Kitengo cha damu salama hospitali ya meta mkoani mbeya kimewataka wananchi mkoani hapa kujitokeza kwa wingi katika suala la uchangia damu ili kuweza kuwasaidia watu mbalimbali.

akizungumza na mbeya greennewsblog ofisini kwake afisa uhamasishaji wa nyanda za juu kusini Charton Meena amesema kuwa damu inahitajika kwa wingi katika hospitali za nyanda za juu kusini kulingana na mahitaji makubwa ya utumiaji wa damu.

Meena amesema kuwa uhitaji wa damu unahitajika kwa wingi kutokana na matukio mbalimbali ya ajali na magonjwa ya akina mama na watoto ambapo husababisha mahitaji ya damu kwa wingi.

Aidha Meena amesema kuwa njia zinazo tumika kuwafikia wananchi ili kuhamasisha kuchangia damu ni kutumia  vipeperushi, mitandao ya kijamii ,vyombo vya habari.

Hata hivyo Meena ameongeza kuwa zipo changamoto mbalimbali katika suala la kuchangia damu ambapo amesema changamoto hizo ni uwoga wawananchi,mila potofu pamoja na imani za kinidi.

         


muonekano wa hospital ya wazazi meta ambapo ndio makao makuu ya damu salaama nyanda za juu kusini

makao makuu ya damu salaama nyanda za juu kusini

Charton Meena





0 comments: