Saturday 23 August 2014

MFANYAKAZI WA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA AJINYONGA

Mwili wa Fredrick Mgaya (60) ukiwa unaning’inia katika mtu aliojinyongea , Tunaomba radhi kwa picha hii.
————————–

Mwanaume mmoja Fredrick Mgaya
(60), mkazi wa Peramiho, Songea mkoani Ruvuma amejinyonga usiku wa kuamkia leo
katika maeneo yaliyo karibu na viwanja vya michezo vya Abasia kijijini
Peramiho. 
  Mwanaume huyo aliyekuwa
akifanya kazi kitengo cha maabara katika Hospitali ya Peramiho na kustaafu
mnamo mwezi aprili mwaka huu amekutwa amejinyonga majira ya asubuhi ya leo.
Marehemu Fredrick Mgaya amekutwa na
ujumbe katika mfuko wa shati lake, ulioelezea chanzo kilichopelekea yeye
kujitoa uhai.
 Afande Allen Urio ambaye alikuwa mmoja wa
mashuhuda wa kwanza,anasema “ Nilikuwa natoka lindo asubuhi ndipo nikakuta
kundi la wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa njiani, nikawauliza kwanini
wamesimama badala ya kwenda shule muda ule, ndipo waliponiambia kuna mtu
ananing’inia kwenye mti pale. Nilipofika kwenye mti huu ndipo nilipomkuta mzee
wetu Fredrick Mgaya akiwa ameshapoteza maisha.
 Ni tukio la kusikitisha sana
kwani ni mzee wetu katika jamii ambaye tulikuwa tunaishi naye vizuri. Mbali na
migogoro yake na mkewe lakini uamuzi aliouchukuwa unasikitisha na si mzuri
kabisa. Kama mlinda amani katika jamii napenda kuwaasa wananchi wajaribu
kutafuta suluhu ya matatizo kwa namna nyingine na sio kwa kujitoa uhai”
Akiongea  Hakimu wa mahakama ya mwanzo kijijini
Peramiho bi Maria Sambo amesema, ameshaletewa na kusuluhisha migogoro ya ndoa
hiyo ya marehemu mara mbili na hadi sasa kuna kesi inayoendelea katika mahakama
ya Hakimu mkazi, lakini  kwa hali ya
kawaida hakudhani kwamba marehemu Fredrick Mgaya angefikia hatua hiyo ya
kujitoa uhai. 
 
Nao mashuhuda wa tukio hilo wakiongea
kwa masikitiko, wengi wamelaani uamuzi uliofikiwa na mzee Mgaya kwani ni
dhahiri alikuwa ni mtu wa watu na pia alikuwa ni tegemeo la familia yake ambayo
amewaacha ghafla. Uamuzi ambao umesababisha maumivu kwa wanajamii hususan
ndugu, jamaa pamoja na marafiki wengi waliokuwa wakimpenda na kushirikiana naye
kwa mambo mengi ya kimaisha.
Mwenyekiti wa kijiji cha Peramiho
A Bwana Joseph Ngonyani ameonesha masikitiko yake ya dhati kwa kuondokewa na
moja ya wazee aliokuwa akiwategemea kwa ushauri katika kijiji chake. “Tukio
hili linagusa sana unajua, kwasababu linahusu mtu wa karibu sana na ambaye
tunashinda nae siku zote bila kujua nini kinamsibu na nini anakipanga katika akili yake”. 
Ndoa nyingi sana zinasumbuliwa na
migogoro ya hapa na pale, hivyo ni vizuri watu wa ustawi wa jamii na asasi
zinazohusiana na jamii kujaribu kutoa mafunzo na maelekezo ya jinsi ya kutatua
migogoro hiyo ili kuepusha adha kama hii isijitokeze tena ndani ya jamii
yetu.Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo bwana Ignasi Kapinga.
 Winfried Thadei Mgaya, mdogo wa marehemu
anasema, amepokea tukio hilo kwa mshtuko na kwa majonzi sana. Anapata uchungu
sana juu ya msiba wa kaka yake kwani marehemu ameacha watoto wanne ambao bado
ni tegemezi pamoja na mjane. Pia amesema mazishi yatafanyika tarehe 7
jumamosi  kijijini kwao Madaba, 
Songea
mkoani Ruvuma.Habari kwa hisani ya Demashonews
 
 
 

0 comments: