MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Wednesday 31 July 2013

WACHEZAJI WA YANGA SC WANADAI CHAO

 
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana Jumatatu. Picha na Michael Matemanga.  
 
 

Siku moja baada ya uongozi wa Yanga kugomea mechi zake kuonyesha na kituo cha Azam TV, jana wachezaji wa klabu hiyo wamelalamika kutopewa fedha za zawadi ya ubingwa.
Mabingwa hao mwanzoni mwa mwezi huu walikabidhiwa Sh70 milioni ikiwa ni zawadi ya ubingwa,  lakini mpaka sasa wachezaji hao hawajalipwa kama walivyoahidiwa.

Wakizungumza na gazeti hilijana kwa sharti la kutotajwa majina yao wachezaji hao walidai wanashangazwa na ukimya uliotawala wa viongozi wao kuhusu haki yao.

“Tunafahamu tayari wadhamini Vodacom wamezitoa fedha hizo, na tulitegemea tungezipata kwa wakati kama zilivyotolewa kwa wakati, lakini inashangaza mpaka sasa ukimya umetawala na wala hatujaambiwa lolote kuhusiana na hilo,” alisema mmoja wa wachezaji hao.

Mwingine aliongeza kuwa kama kweli uongozi umeridhia kuwakabidhi fedha hizo ni vyema wakafanya kwa muda huu wakati wakijiandaa na msimu mpya wa ligi kwani kwa kutofanya hivyo kutachangia kupunguza morali yao na wengine kucheza chini ya kiwango.

“Inashangaza eti tuanze msimu mpya wakati hata fedha za ubingwa msimu uliopita hatukupewa hii ina maana gani kwetu? Ni vigumu wachezaji wakacheza kwa moyo wakati wanaona hawajatendewa haki, uongozi uliangalie jambo hili kwa mapana na kulifanyia kazi kwani sisi pia tuna familia zinatutegemea,” alisema mwingine.

Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako aiimbia Mwananchi kuwa ni kweli wachezaji hao hawajapewa fedha, lakini watalipwa kwa muda mwafaka.
“Kila kitu kina taratibu zake hatuwezi kupokea fedha na kuwapa wachezaji, wavute subira hata sisi tunafahamu umuhimu wa kuwapa haki yao, watafanyiwa sherehe na kukabidhiwa fedha hizo”  alisema.

Mbali ya fedha hizo pia wachezaji hao wanadai kutolipwa ahadi yao waliyopewa ya Sh100 mil kama wataifunga Simba na kutwaa ubingwa msimu uliopita.  Hata hivyo habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema moja wa kiongozi wa juu wa timu hiyo amechukua fedha zote za zawadi ya ubingwa kwa lengo la kufidia deni lake analoidai timu hiyo.
 
CHANZO 
Na Jessca Nangawe, Mwananchi
Posted  Jumatano,Julai31  2013 

WALIONACHO WANASAMEHEWA KODI,WASIONACHO WANAKAMULIWA......'''''''''''''

 
 
 

Wiki iliyopita katika safu hii nilijadili suala la kuanzishwa kwa kodi za simu katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu.
Ni jambo linaloonekana kuichanganya Serikali hasa baada ya malalamiko ya wananchi, maana kila kiongozi anasema lake. Waziri wa Fedha anasema hivi, Rais anasema vile, Waziri Mkuu anasema lake, chama tawala kinasema vile! Huu ni mwiba.


Siyo kwamba napinga kulipa kodi. Hapana. Hakuna Serikali kokote duniani isiyotoza kodi wananchi wake. Idadi ya watu katika nchi yoyote ni rasilimali ya maendeleo kwani kama watu hao watalipa kodi kikamilifu, basi Serikali itakuwa na fedha za kutosha katika maendeleo.

Tatizo linakuja pale walipa kodi wakubwa wanaposamehewa halafu wale wasionacho wanabambikwa kodi maradufu.
 Hata hivyo, wakati Serikali inahimiza wananchi wa chini kulipa kodi, hata kutoka   kwenye chanzo ambacho si mapato kama simu, kuna misamaha mingi ya kodi inayotolewa kwa walipa kodi wakubwa hasa wawekezaji.

Kwa mfano katika sekta ya madini, Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC), inatoa misamaha lukuki ya kodi kama kivutio kwao.
Kulingana na cheti cha vivutio hivyo ni pamoja na kufutwa kabisa kodi kwenye mafuta ya mitambo na magari (ikilinganishwa na Sh200 kwa lita wanayolipa raia) kwa muda wote wa utafutaji madini na mwaka mmoja wa kwanza wa uzalishaji ambapo watalipa asilimia tano tu.

Misamaha mingine ni kwenye mapato juu ya mtaji, msamaha wa kulipa VAT kwa kuagiza bidhaa nje ya nchi na hata ndani.
Vilevile kampuni hizo hulipia kodi ya stempu kwa asilimia 0.3 tu kinyume cha sheria inayoitaka kuwa asilimia nne.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) misamaha ya kodi iliyotolewa kwa kampuni za uchimbaji madini pekee kwa mwaka 2011 ilikuwa Sh109.885 billioni huku misamaha iliyotolewa na TIC ikifikia Sh239.667 billioni. 

Hii ndiyo sababu ya umaskini kuendelea nchini licha ya kuwa rasilimali nyingi yakiwamo madini. Ndiyo maana hata mikataba ya madini inafanywa siri kubwa.


Huo ni mfano mmoja wapo. Ipo mianya mingi tu ya ukwepaji wa kodi. Siyo kwa bahati mbaya ila ni kwa makusudi. Mbali na misamaha, tumesikia mara kadhaa, baadhi ya viongozi wa Serikali wakificha mabilioni ya fedha nje ya nchi. Kwa mfano zile Sh300 bilioni zilizofichwa Uswizi zimeishia wapi? Afadhali tulifanikiwa walau kupata chenji ya rada kwa msaada wa Uingereza, lakini waliohusika na mchezo ule mbona hawaguswi?
Hayo yote bado ukamkamue mwananchi wa kawaida Sh1,000 ya simu kwa mwezi?

 CHANZO mwananchi gazeti
 Posted  Jumatano,Julai31  2013  saa 12:42 PM

MTANZANIA ATIMULIWA KWA AIBU BIG BROTHER AFRIKA

 

Nando. 

MSHIRIKI machachari katika mashindano ya Big Brother The Chase, Amil Khan maarufu kama Nando, juzi Jumapili usiku alitimuliwa kwenye jumba hilo baada ya kuingia na mkasi chumbani alipogombana na Elikem wa Ghana hali iliyowafanya waandaaji kuingiwa hofu.


Akizungumza na Mwanaspoti, Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi alisema ofisi yake imepokea taarifa hizo na kwamba mwakilishi huyo wa Tanzania alivunja masharti ya mchezo huo kwa kuhatarisha uhai wa mshiriki mwenzake Elikem.

“Nando amekuwa na tabia ya kubeba vitu hatarishi mara kwa mara, waandaaji wa mashindano walituvumilia kwa mara ya kwanza alipokutwa na kisu kwenye sherehe ya Channel O mwezi uliopita, lakini baadaye amegombana na mwenzake anaahidi kumuua, ule mkasi aliobeba kwenda nao chumbani ni kithibitisho,” alisema Kambogi.


Kambogi alisema bado haijafahamika rasmi ni lini Nando atarejea nchini kwani kwa sasa lazima atafutiwe mwanasaikolojia ili aweze kurudishwa katika hali yake ya kawaida.


Kabla ya kugombana na Elikem, Ijumaa iliyopita, Nando amekuwa na tabia ya kubeba vitu vya hatari mfukoni akiwa kwenye sherehe mbalimbali zilizokuwa zikifanyika ndani ya jumba hilo.

Baada ya kukutwa na kisu mwezi uliopita kwenye sherehe ya Channel O, Biggie(kiongozi wa jumba) alimwita na kumpa onyo la kwanza, lililohusu ukiukwaji wa sheria za mashindano kwa kutembea na silaha.


 chanzo mwanasport
By HERIETH MAKWETTA  
  Jumanne,Julai30  2013

MENGI YAIBUKA MTOTO ALIYETUPWA ENEO LA NDIUKA ''A'' MKOANI IRNGA

 

Mwenyekiti  wa serikali ya mtaa wa Ndiuka  A Siwema  Ally  akisoma barua  aliyoandikiwa  mwanamke huyo na polisi Makambako







SIKU  moja baada ya mwanamke  aliyetambuliwa  kwa  jina la Stella Mnyagani mwenyeji  wa Mabadaga Chimala wilaya ya  Mbarali mkoa  wa  Mbeya  atelekeza  mtoto  wake  wa  kiume  nje ya  duka  moja  eneo la Ndiuka  'A' katika Manispaa ya  Iringa.

Mengi  yafichuka  juu ya mwanamke  huyo  kutelekeza  mtoto  wake inasadikika  mwanamke  huyo alikuwa akifanya kazi ya  kuuza bar  katika  eneo hilo la Ndiuka na baadhi ya maeneo ya mji  wa Iringa.
Mashuhuda  waliobahatika  kumwona mwanamke  huyo  wanadai kabla ya  kutenda  unyama  huo  wa kutupa mtoto  mwanamke  huyo alikutwa katika mitaa mbali mbali ya mji  wa Iringa likiwemo eneo la Ofisi za Tanesco  akiwa amekaa kando ya  barabara  kabla ya  kuondoka  na kuelekea  eneo la Ndiuka ambako aliamua kumtekeleza mtoto  huyo .

Mtoto  huyo  wa  kiume anayekadiliwa  kuwa na  mwaka  mmoja alikutwa  juzi majira ya saa 2 usiku katika  eneo hilo la Ndiuka  'A' huku  akiwa na vifurushi  viwili  vya nguo  pamoja na dawa  za aina  mbali mbali .

Mwenyekiti  wa  serikali ya  mtaa  huo  wa Ndiuka  A Siwema  Ally  alisema  kuwa  mtoto  huyo  aliokotwa na  wasamaria  wema na kupelekwa  kwake  kabla ya  kuchukuliwa na  polisi na  kupelekwa  kituo cha yatima  cha Daily  Bread Life MInistries kinachomilikiwa na Neema Mpeli

Mwanamke  huyo pia  aliacha namba  za  simu ambazo ni  0766663281 inayomilikiwa na Kastori Mlyatage  pamoja na namba  ya Mahenge  wa  Mabadaga  0753493063  na  namba ya mama  Fatuma  0757 519270 pamoja na barua  inayoonyesha  alisaidia  kituo cha  polisi Makambako  kwa  ajili ya Kwenda Singida

 
 
 
CHANZO na GODWINFRANCES BLOB

CHADEMA YAVUNA WANACHAMA 300 TANGA

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Tanga kimepata wanachama wapya zaidi ya 300.
Wanachama hao wamepatikana katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika wilaya za Handeni, Muheza na Korogwe uliohutubiwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje.
 
Wanachama 220 wamejiunga na chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kwengoma, Kata ya Kwamatuku, Wilaya ya Handeni na wanachama 71 ni kutoka Kibanda, wilayani Muheza.
Wanachama wengine 21 akiwamo mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Turiani, Bakari Kimea walijivua uanachama wa CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kwashemshi, Wilaya ya Korogwe.
 
Wakizungumza katika mikutano hiyo baada ya kujiunga na CHADEMA, walisema wameamua kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa kimeshindwa kuondoa kero zinazowakabili kwa miaka mingi.
Miongoni mwa kero hizo kwa mujibu wa wananchi hao ni unyanyaswaji unaofanywa na viongozi wa serikali za vijiji, kunyang’anywa ardhi, kero ya maji na kuvunjiwa mikataba na muwekezaji. 
 
CHANZO chademablog.com

HATIMA YA KESI YA MAKADA WA CHADEMA AUGOST 5

 
 
Uamuzi dhidi ya kesi inayowakabili wanachama watano wa Chadema yaliyokuwa yatolewe jana sasa yatatolewa Agosti 5. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Simon Lukelelwa alitoa uamuzi huo kufuatia kuchelewa kufika kwa washtakiwa wa kesi hiyo waliohifadhiwa Gereza la Uyui Tabora.
Wakati uamuzi huo ukitolewa na Jaji Lukelelwa, washtakiwa wote watano wa kesi hiyo, Henry John Kileo, Evodius Justian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta na Rajab Kihawa hawakuwa katika chumba cha mahakama muda wa saa tatu na nusu asubuhi.
Washtakiwa walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa nne na dakika arobaini na waliarifiwa na wakili mwakilishi, Emanuel Msyani kuwa shauri limepangwa tarehe tano mwezi ujao wakiwa ndani ya chumba cha mahabusu ya Mahakama Kuu.
Wakili Msyami alisema Mahakama Kuu iliridhia ombi la upande wa Jamhuri kuomba kuongezewa muda angalau kwa siku moja kwa vile walipokea hoja Ijumaa iliyopita.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ilikubali ombi hilo na kuongeza muda hadi tarehe moja uwe umewasilisha majibu ya hoja na kuipanga tarehe tano kwa ajili ya uamuzi.
Kesi hiyo ya rufaa ya jinai namba 53/2012 ilifunguliwa na Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala na kuanza kusikilizwa Julai 22 mwaka huu mbele ya Jaji Lukelelwa ikiomba miongozo ya kisheria ikiwemo yaliyotolewa na mahakama za wilaya na mkoa.
Shauri la maombi ya marejeo liliwakilishwa na Wakili Peter Kibatala anayewatetea washitakiwa, akiiomba mahakama kuu ipitie majalada ya kesi mbili dhidi ya wateja wake zilizofunguliwa mahakama hizo baada ya kuona maamuzi yake hayakutenda haki.
Wakili Kibatala alibainisha katika maombi hayo kwamba kutokana na maamuzi hayo ya mahakama za chini yameathiri pia haki za waomba rufaa ikiwa ni pamoja na kuwanyima haki ya kupata dhamana.
Kwa upande wake Serikali ilishindwa kujibu maombi hayo, badala yake ilijenga hoja kwamba walichelewa kupata nyaraka hizo kwani walizipokea siku moja kabla ya kutajwa shauri hilo hivyo walishinda kuzijibu.

Tuesday 30 July 2013

TUTAMSHITAKI WAZIRI MKUU MAHAKAMANI LHRC


LHRC: Tutamshtaki Waziri Mkuu mahakamani

 

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda 



kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”

Alijibu: “Ni lilelile nililosema... Mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... Hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria. “Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... Wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... Maana tumechoka.”



Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema jana wakati akitoa ripoti ya utafiti ya miezi sita kuhusu mambo mbalimbali ya haki za binadamu kuwa kituo hicho kiko katika hatua za mwisho za kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu ili kumfungulia kesi Waziri Mkuu.

“Kauli ya Pinda inavunja Katiba ya nchi ya usawa mbele ya sheria ambayo ni Ibara ya 13 (1). Hivyo tumekusudia kumfungulia kesi Waziri Mkuu ambaye amevunja Katiba,” alisema.

Sungusia alisema kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi wa juu wa Serikali ni kinyume cha Katiba, sheria za nchi na misingi ya haki za binadamu hivyo.


“Pinda alitoa kauli ile kama msimamo wa Serikali, tulitarajia angefuta kauli yake aliyotoa bungeni ya kuwabariki polisi kupiga raia katika mkutano ulioisha wa Bunge la Bajeti lakini hakufanya hivyo,” alisema.

Ofisi ya Waziri Mkuu wajibu

Akizungumza madai hayo jana, Katibu wa Waziri Mkuu, Deusdedit Buberwa alisema: “Hayo unayoniambia ni mapya kabisa. Mimi sifahamu chochote, kwani sijaona hata barua yao. Ningeweza kuzungumza kama ningepata barua au hata kusikia, lakini hakuna hicho kitu.”

Utafiti wa mauaji


Akitoa taarifa ya utafiti huo, Mtafiti wa LHRC, Pasience Mloe alisema katika kipindi cha miezi sita mwaka huu, kumekuwa na vifo 303 vilivyotokana na imani za kishirikina.

Alisema idadi hiyo ni kubwa kwani inakaribia sawa na takwimu za mwaka mzima wa 2012 ambao watu 336 walipoteza maisha kwa sababu hizohizo.

Mloe alisema utafiti huo ulibaini kuongeza kwa ubakaji wa watoto kwani katika kipindi hicho cha miezi sita, 394 walifanyiwa ukatili huo.

MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA NA KUMPA MIMBA MTOTO WAKE

Mkazi mmoja wa Isanga, Mbeya amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba binti yake wa kumzaa wa umri wa miaka 15.



MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa).



Mwendesha mashitaka wa serikali  Archiles Mulisa  aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.



Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho  mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya kuzini.


akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.

Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito Mei, 2012.

Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.

Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.

Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa  Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.

Aidha kabla ya kutoa hukumu Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.

Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.

Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “ mfa maji haachi kutapatapa”

Na Mbeya yetu

 
     

Monday 29 July 2013

MFANYAKAZI WA MWANANCHI COMMONICATION LIMITED APIGWA RISASI

 
  . Picha na Venance Nestory 

Na Daria Erasto, Mwananchi  
Posted  Jumatatu,Julai29  2013


Dar es Salaam. Watu ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi wamemjeruhi kwa risasi mfanyakazi wa Idara ya Usambazaji ya Mwananchi Communications Limited,  Jackson Ngassa.

Tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi saa 4 usiku eneo la Tabata Matumbi baada ya watu hao kumfuatilia Ngassa tangu alipokuwa anatoka ofisi za Mwananchi eneo la Tabata Relini.


Akizungumza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (Moi), Ngassa alisema wakati akitoka ofisini siku hiyo aliona pikipiki tatu zikiwa nyuma yake lakini hakuhisi kama zilikuwa zinamfuata mpaka walipofika taa  za kuongozea magari za Tabata Dampo.

“Nilipofika Tabata Dampo nilihisi kufuatiliwa kwa sababu kila nilipopunguza mwendo nao walipunguza mpaka nilipofika Matumbi ndipo nikasikia wakiniambia simama haraka na kisha wakapiga risasi moja ambayo ilitoboa tanki la mafuta la pikikipiki,” alisema Ngassa.

Alisema baada ya kuona hivyo akataka kukimbilia Benki ya Access iliyoko eneo hilo la Matumbi lakini kabla hajafanya hivyo pikipiki nyingine ilimzuia kwa mbele na ghafla akasikia risasi ambayo ilipasua sehemu ya goti mguu wake wa kulia.


Hata hivyo, Ngassa alisema begi hilo halikuwa na pesa zozote zaidi ya  kadi ya benki na magari ya kuchezea watoto aliyowanunulia watoto wake.

Kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kuunganisha mifupa iliyovunjika kwani risasi aliyopigwa iliingia na kutoka upande wa pili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari alikwisha mtembelea majeruhi katika hospitali ya Muhimbili alikolazwa.


DK SLAA AMWEKA KITIMOTO DK NCHIMBI

 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akichangia hoja kwenye Kongamano la Kujadili Amani nchini kwa miaka 50 ijayo lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis Felix 
Na Raymond Kaminyoge, Mwananchi  
Posted  Jumatatu,Julai29  2013  


Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi jana alikuwa na wakati mgumu katika Kongamano la Amani lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa kumtaka ajiuzulu kutokana na kushindwa kudhibiti uhalifu nchini.

Mbali ya Dk Nchimbi, Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi katika kongamano hilo, Brigedia Jenerali, Elias Athanas naye alibanwa akitakiwa kueleza tuhuma za askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kuhusishwa na vitendo vya ubakaji na utesaji wa raia mjini Mtwara.

Akizungumza katika kongamano hilo, Dk Slaa alisema hakuna haja ya kutafuta mchawi wa amani ya nchi bali, Serikali inapaswa kulaumiwa kutokana na watendaji wake kushindwa kuwajibika ipasavyo.
Alitoa mfano wa kitendo cha Bandari ya Dar es Salaam kutumiwa kupitisha pembe za ndovu wakati maofisa polisi wakiwemo ni kitendo cha aibu ambacho kinatosha kumfanya Waziri Nchimbi ajiuzulu.

Akijibu madai hayo wakati akihitimisha kongamano hilo, Waziri Nchimbi alikiri kuwa baadhi ya polisi wamekuwa na tabia ya kujihusisha na rushwa na katika kupambana na hali hiyo, Serikali imeshawatimu kazi askari 101  katika kipindi cha mwaka 2012.
Hata hivyo, Dk Nchimbi alisema suluhisho la matatizo yaliyopo ndani ya Jeshi la Polisi siyo kuwatimua kazi askari pekee na ndiyo maana Serikali imeanza mkakati wa kutoa mafunzo ya maadili ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa weledi.

Alisema ataendelea kupokea changamoto kutoka kwa wadau wote wa amani na kupongeza waliobuni kongamano hilo, huku akiahidi kutoa ushirikiano kufanikisha jambo lolote linalohusiana na mjadala wa amani ya nchi.
Kuhusu ubakaji na utesaji wa wanajeshi, Dk Slaa alisema inasikitisha kuona jeshi ambalo linapaswa kulinda amani linatesa na kuwabaka raia.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alisema anao ushahidi wa wanachama wa chama chake waliojeruhiwa na kupakwa pilipili akisema kwamba jeshi hilo limekuwa na baadhi ya askari wakatili tofauti na misingi ya kuanzishwa kwake.

Akijibu tuhuma hizo, Brigedia Jenerali Athanas alikanusha madai hayo akisema siyo kweli kwamba JWTZ linaendesha unyama na kwamba lipo Mtwara kwa ajili ya kulinda amani na kusema tuhuma hizo ni za mitaani.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alidai kuwa tangu nchi ilipopata uhuru haijawahi kuwa na amani ya kweli akitoa mfano wa wananchi kuhamishwa kwa nguvu katika maeneo yao.

Alisema katika siku za karibuni, tofauti na zamani polisi ilipokuwa ikifanya kazi ya kudhibiti uhalifu, sasa inaonekana kama kazi yake ni kudhibiti upinzani na limekuwa likituhumiwa mara kwa mara kwa kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na kusababisha mauaji.

 CHANZO  MWANANCHI GAZETI

WALIOGOMA KURUDIA KDATO CHA 2 KUKIONA

 


SERIKALI imewataka wazazi kuhakikisha wanafunzi wote 36,000 waliofeli kidato cha pili mwaka jana na kutakiwa kurudia darasa hilo wanafanya hivyo vinginevyo hawataruhusiwa kufanya mtihani wa kidato nne mwakani.
Tahadhari hiyo ilitolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, wakati akifungua mafunzo ya Waratibu Elimu kata Kitaifa yaliyoendeshwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo, Pwani.

Mulugo alisema kuna taarifa ya kuwepo kwa baadhi ya wanafunzi hao kushawishiwa na wakuu wa shule pamoja na wazazi wao kuendelea na kidato cha tatu kwa matumaini ya kuwa watafanya mitihani ya kumaliza kidato cha nne mwakani, jambo aliloeleza kuwa halitawezekana.

Aliwaagiza Waratibu Elimu Kata nchini kufanya utaratibu wa kufuatilia mara moja wanafunzi wote wa kidao cha pili waliofeli kama wamekariri darasa hilo kama ilivyoagizwa na wizara na endapo watawabaini waliokaidi watoe taarifa mapema, ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Awali, Ofisa Taaluma wa Mkoa wa Dar es Salaam, Benadeta Thomas, alisema mafunzo hayo yanaendeshwa katika mikoa 11 nchini na ni utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari ngazi za kata na kwamba mikoa inayohusika ni Dar es Salaam, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Kilimanjaro, Singida, Ruvuma, Arusha, Tabora, Mwanza na Tabora

na Julieth Mkireri, Bagamoyo TANZANIA DAIMA

IDD AZAN AZUNGUMZIA TUHUMA ZA KUFANYA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA

Picture: Idd Azzan
IDD AZAN
Siku chache baada ya jina lake kutajwa kwenye waraka unaodaiwa kuwa barua kutoka kwa mmoja wa  Watanzania waliofungwa katika jela huko Hong Kong, Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan amezungumza na kusema kuwa yupo tayari kujiuzulu ubunge ikiwa itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya.
 
Idd Azzan amekaririwa na HabariLeo (via) jana akisema kuwa hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla. Akasema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake amedhamiria kumshushia heshima na huenda ana jambo limejificha.

Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.



Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwa nini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo?

Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa hayupo nje ya nchi, kwani 


katika maelezo yake anataja jina la Balozi Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa Shirikisho la Ujerumani.

Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernard na kukatwa kwa wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo tayari kujiuzulu ubunge wangu.

Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu.

Sijawahi kuuza dawa za kulevya na hata katika familia yangu hakuna mtu anayefanya biashara hiyo haramu. Kila mmoja anajua kuwa Idd nilikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni, huku kazi yangu kubwa ikiwa ni biashara ya magari na daladala ambayo ninaendelea nayo hadi sasa mbali ya ubunge kama nilivyopewa heshima na wapiga kura wangu wa Kinondoni.

Alipoulizwa kuwa ni hatua gani ikibainika hakuna ukweli wa jambo hilo baada ya vyombo vya usalama kufanya uchunguzi, Azzan alisema: “Ni ngumu kusema hatua gani nitachukua ikibainika hakuna ukweli, lakini nataka kusema kama yule aliyeandika barua hii angetaja jina lake ni wazi baada ya uchunguzi ningeweza kuomba ushauri kwa mwanasheria wangu hatua za kuchukua, lakini kwa kuwa hakutaja jina ni ngumu kuweza kuamua.” 

Source:  habarileo gazeti

Saturday 27 July 2013

JAPHET KASEBA AIANGUKIA SERIKALI

 
BONDIA wa ngumi za mateke ‘Kick boxing’, Japhet Kaseba, ameisihi serikali kuwekeza kwenye mchezo huo na sekta hiyo kwa ujumla ili iweze kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji mbalimbali.

Kaseba anayeing’arisha Tanzania katika ndondi aina ya Kick Boxing, alisema juzi kuwa kama serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, ingefanya uwekezaji kwenye sekta hiyo, ingetoa ajira kwa vijana wengi.
“Tanzania imejaliwa kuwa na vijana wengi wenye vipaji, lakini vimekosa sapoti ya serikali, tungekua na serikali inayojali na kuthamini michezo kwa vitendo, sekta ya michezo ingekuwa msaada kwa vijana wengi,” alisema.

Kaseba anatoa pia wito kwa mabondia chipukizi kuwa wavumilivu katika kujifunza mchezo huo licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi zinazoweza kuwavunja moyo.
“Kinachotakiwa kufuatwa katika mchezo huu ni nidhamu, bondia akiwa na nidhamu pamoja na kufuata sheria zote za mchezo huo atafanikiwa,” alisema.


na Mwandishi wetu  Tanzania dima

AFISA FEKI WA NIDA AKAMATWA NA POLISI

 


JESHI la Polisi mkoani Dodoma, linamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za utapeli kwa kuwadanganya wanafunzi wa vyuo vikuu, kuwa atawapatia kazi Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime, alisema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia majina tofauti ambayo ni Mariam Tawakali na Monica Ngaso (28).

Alisema hadi sasa mwanamke huyo amewatapeli wahitimu wa vyuo vikuu 29 ambapo kila mmoja alikuwa akitoa kiasi cha sh milioni 2.9 kwa madai ya kuwapatia kazi ya kuandikisha wananchi katika zoezi la vitambulisho vya taifa.

“Mwanamke huyo alikamatwa Julai 25 mwaka huu katika mtaa wa Barabara ya Sita katika Maniaspaa ya Dodoma.
“Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa kuna mwanamke anajitambulisha kwa baadhi ya wananchi kwamba anafanya kazi katika Manispaa ya Dodoma na anajishughulisha na zoezi la NIDA la uandikishaji wa vitambulisho vya taifa,” alisema.

Misime alisema mtuhumiwa huyo aliwatangazia wananchi kwamba zoezi hilo kwa mkoa wa Dodoma litaanza Agosti 2013 na kwamba kila anayehitaji kazi hiyo awasilishe maombi kwake.

Alisema maombi hayo yalitakiwa kuambatanishwa na vyeti vya sekondari au chuo, picha na fedha tasilimu sh 110,000 kama kiingilio.
“Mtuhumiwa aliwaambia waombaji hao kwamba ambaye angepata nafasi ya kufanya kazi angelipwa sh 400,000 kwa mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo kazi hiyo ingekuwa imekamilika,” alisema.

Misime alisema mtuhumiwa alikamatwa na vyeti 29 vingi vikiwa ni vya wanafunzi waliohitimu vyuo vikuu mwaka huu.
Alitoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na watu wanaofanya vitendo hivyo. Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani. 


IMEANDIKWA  na Danson Kaijage, Dodoma tanzania daima

ANGALIA ORODHA YA MISHAHARA MIPYA YA WATUMISHI WA UMMA 2013

TGHS I (Sh 2,800,000).

TGHS J
Picture: Tanzanian coins shilling

TGHS J (Sh 2,900,000)

TGHS K

TGHS K (Sh 3,100,000)

TGHS L

TGHS L (Sh 3,400,000)

Watumishi wa Mahakama

TJS 1

TJS 1.1. (Sh 510,000), TJS 1.2. (Sh 535,000), TJS 1.3. (Sh 560,000), TJS 1.4. (Sh 585,000), TJS 1.5. (Sh 610,000), na TJS 1.6. (Sh 635,000) na TJS 1.7. (Sh 660,000).

TJS 2

TJS 2.1. (Sh 770,000), TJS 2.3. (Sh 805,000), TJS 2.3. (Sh 840,000), TJS 2.4. (Sh 875,000), TJS 2.5. (Sh 910,000), TJS 2.6. (Sh 945,000), na TJS 2.7. (Sh 980,000).

TJS 3

TJS 3.1. (Sh 1,075,000), TJS 3.2. (Sh 1,115,000), TJS 3.3. (Sh 1,155,000), TJS 3.4. (Sh 1,195,000), TJS 3.5. (Sh 




1,235,000), TJS 3.6. (Sh 1,275,000), na TJS 3.7. (Sh 1,315,000).

TJS 4

TJS 4.1. (Sh1,420,000), TJS 4.2. (Sh 1,470,000), TJS 4.3. (Sh 1,520,000), TJS 4.4. (Sh 1,570,000), TJS 4.5. (Sh 1,620,000), TJS 4.6. (Sh 1,670,000), na TJS 4.7. (Sh 1,720,000).

TJS 5

TJS 5.1. (Sh 1,805,000), TJS 5.2. (Sh1,875,000), TJS 5.3. (Sh 1,945,000), TJS 5.4. (Sh 2,015,000), TJS 5.5. (Sh 2,085,000), na TJS 5.6. (Sh 2,155,000).

TJS 6

TJS 6.1. (Sh 2,250,000), TJS 6.2. (Sh 2,350,000), TJS 6.3. (Sh 2,450,000), TJS 6.4. (Sh 2,550,000), na TJS 6.5. (Sh 2,650,000).

TJS 7

TJS 7 (Sh 3,560,000)

TJS 8

TJS 8. (Sh 4,050,000)

TJS 9

TJS 9. (Sh 4,480,000)

TJS 10

TJS 10 (Sh 4,600,000)

Kwa viwango vingineb bovya hapa www.wavuti.com

NGUZO ZINAZO OZA AU KUANGUKA NI HATARI KWA WANANCHI (ANGALIA HII NGUZO)

Hii nguzo iliyooza inamsubiri muda ufike ifunge barabara au imwangukie mtu imuue.

Hii nguzo ilianguka usiku wa manane na hadi saa 3 asubuhi ya leo Jumamosi tarehe 27/07/2013 hakuna mtu yeyote wa TANESCO aliyefika kufanya chochote. Nguzo hii iko barabara ya kutokea mzunguko wa Kijenge kuelekea Philips maeneo ya ofisi za KK security na iliyokuwa Sabasaba Hotel.

Itakapoanguka katikati ya barabara itasababisha msongomano mkubwa sana kwani hii barabara ina traffic kubwa.

Hivi ni kwa nini hadi sasa hamna mtu anayeshughulika ilihali umeme umekatika na Meneja wa TANESCO Arusha akiendelea kuuchapa usingizi wa Jumamosi?

Nguzo hii inaonekana imeoza na huu ni uzembe mkubwa kwani TANESCO kila wakati wanatumia fedha nyingi kuboresha miundombinu.

 

Source:  MVUMBUZI

STARS KUPAMBANA NA UGANDA THE CRANES LEO ( ANGARIA MANDARI YA STARS)

STARS WAKIWA MAZOEZI KUPAMBANA NA CRANE LEO




 
Wachezaji mbalimbali wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Satrs' ambao wanasakata kabumbu ndani ya nchi wakijifua katika Uwanja wa Taifa wa Mandela uliopo Nambole nchini Uganda. Stars ipo nchini Uganda na leo inataraji kushuka katika dimba la uwanja huo kumenyana vikalina The Crenes ya Uganda kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani CHAN.

Moja ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya leo (Julai 27 mwaka huu) dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.
 

Friday 26 July 2013

ATUHUMIWA KWA SHITAKA LA KUMUA MUMEWE ILI ARIDHI MALI


PictureJaneth Jackson (32), mke wa mfanyabashara maarufu wa madini mkoani Arusha anadaiwa  kupanga njama za kumuua mumewe wa ndoa na mtoto wa mume huyo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, amesema mwanamke huyo aliwaagiza watu wawili kumsaidia kutekeleza azma yake hiyo ya kumuangamiza mumewe, mtoto wake na ndugu wanaoweza kumzuia urithi.

Kamanda Sabas, amesema Julai 16 mwaka huu majira ya saa mbili usiku, jeshi la polisi lilipokea taarifa kutoka kwa mfanyabiashara huyo kuhusu kuwepo mpango ulioandaliwa  na mke wa mfanyabiashara huyo wa kumuua yeye na mwanaye na ndugu wa mume  waishio mkoani Kagera ili aweze kumiliki mali.

Amesema katika mpango huo ulioandaliwa na mke wa mfanyabiashara huyo alituma watu wawili kutoka jijini Arusha, eneo la Moshono  kwenda mkoani Kagera ili kufanya mauaji hayo na kisha wangelirejea jijini Arusha ili kukamilisha mpango huo kwa kumuua mfanyabiashara huyo.

Amesema jeshi la polisi lilituma makachero wake na Julai 17 mkoani Kagera ili kufuatilia tuhuma hizo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Novatus Elias Mrisha, kabla ya kutekeleza mpango huo huku mwenzake akikimbia na wanaendelea kumsaka.

Kamanda Sabas amesema kuwa katika mohojiano na Mrisha, mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika katika mpango huo baada ya kutumwa na mke wa mfanyabiashara huyo

Jana, mwanamke huyo ambaye ni mkazi wa Moshono Jijini Arusha alipandishwa katika mahakama ya wilaya ya Arusha iliyopo Sekei, pamoja na mtuhumiwa Novatus Elias Mrisha, jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha/Arumeru, Devotha Kamuzora na kusomewa makosa mwili ya kula njama ya kutaka kumwua Simon Jackson Manjuru Kaijage.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Edna Kasala alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa wote wawili walitenda kosa la pili la kula njama na kutaka kumwua Desderi Sabas (12) ambaye ni mtoto wa nje wa mume huyo anayeishi Bukoba mkoani Kagera.

     
CHANZO WAVUTI.COM

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAUAJI YA MFANYAKAZI WA MGODI WA TANZANIE, KITALU C, MIRERANI WILAYANI SIMANJIRO

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAUAJI YA MFANYAKAZI WA MGODI WA TANZANIE, KITALU C, MIRERANI WILAYANI SIMANJIRO

Tarehe 20 Julai, 2013 kulitokea mauaji ya mfanyakazi wa mgodiwa Tanzanite ulioko kitalu C, Mirerani wilayani Simanjiro kwakupigwa risasi na mchimbaji kutoka mgodi wa wachimbaji wadogowa kitalu D katika eneo hilo.

Kitendo hicho kimetokana na wachimbaji wadogo wanaopakanana Kitalu C kuvuka mipaka ya vitalu vyao na kuendesha uchimbajindani ya Kitalu C, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Madiniya Mwaka 2010 na Kanuni zake.

Kwa sasa Kitalu C kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Madinila Taifa (STAMICO) na Kampuni ya Tanzanite One kwa asilimia 50kwa 50. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika. Wizara imesikitishwa sana na mauaji hayo ambayo ni ukiukwaji wataratibu za usalama migodini.

Serikali haitavumilia kuona vitendo hivyo vikiendelea nakuhatarisha usalama wa wachimbaji katika migodi ya TanzaniteMirerani.

Tunapenda kuwatangazia wamiliki wa migodi yote ya wachimbajiwadogo katika vitalu B na D ambayo uchimbaji wake unafanyikandani ya mipaka ya Kitalu C kuwa wasitishe shughuli zao mara moja
na wahakikishe kuwa uchimbaji unafanyika ndani yamipaka ya vitalu vyao.

Aidha, uchimbaji uzingatie taratibu za usalama migodini ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na utumiaji wa silaha za aina yoyote migodini. Ukaguzi wa migodi kubaini migodi inayoendeshauchimbaji ndani ya mipaka ya kitalu C utafanywa na Timu yawataalam wa Wizara ya Nishati na Madini. Vitalu vitakavyobainika kuhusika leseni zake zitafutwa na uchimbaji utatakiwa kusitishwakatika migodi hiyo.

IMETOLEWA NA,
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
26 JULAI, 2013

Wednesday 24 July 2013

MFUASI WA MUNGUGI AJITIA KITANZI KITANZI AKIHOFIA KUKAMATWA NA POLISI

Maina Njenga na Mithika Linturi
Aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga kwenye picha ya awali. Picha/MAKTABA  

MFUASI sugu wa kundi haramu la Mungiki alijiua kwa kujitia kitanzi usiku wa kuamkia Jumatano Katika Kaunti ya Murang’a baada ya kupata habari kuwa polisi walikuwa wakimwandama.

Bw Peter Gitau wa miaka 23 kutoka kijiji cha Ngaiko anadaiwa kuwa alihofia kukamatwa na kushtakiwa na sheria mpya za kupambana na makundi haramu ambazo zingemwelekeza korokoroni kwa miaka 14 ama faini ya Shilingi Milioni moja ama zote mbili.

Mwili wake ulipatikana na jamii yake ukiwa umening’inia nyumbani mwake na kamba shingoni.

Katika ujumbe aliouacha, kijana huyo alimlaumu aliyekuwa mwenyekiti wa kundi hilo Bw Maina Njenga kwa kuwapotosha vijana wajiunge na kundi hilo na kisha akawasaliti kwa kuwatema ili ajiokoe yeye mwenyewe.

“Yeye alitwambia tujiunge na kundi hilo ili tujitafutie riziki kutoka kwa steji za matatu na pia kwa vituo vya biashara. Baada ya kumkusanyia ushuru huo na kumtajirisha, alijiunga na serikali hiyo na kutuacha mikononi mwa serikali tuuawe na wengine wafungwe,” ujumbe huo ukasema.



Kwa mujibu wa jamii yake iliyoongea na Taifa Leo Bw Gitau alihofia kuwa hatima yake ingekuwa sheria hizo au kuuawa na maafisa wa polisi ambao wanasaka wafuasi wa kundi hilo kote nchini kufuatia tangazo rasmi la Inspekta Mkuu wa Polisi Bw David Kimaiyo.

Jamaa hao walifichua kuwa Gitau aliacha ujumbe huo aliokuwa ameuandika kwa karatasi akiaga jamii yake kwaheri huku akihimiza wafuasi wa kundi hilo waliteme na watii sheria.




“Hatima yangu ilikuwa tu kufungwa ama kuuawa na serikali. Na kwa vile mimi sitaki kuwatwika wazazi wangu jukumu la kuuza shamba ili waninasue kutoka kwa makali ya serikali, nimeonelea nijipumzishe kwa hiali,” ujumbe huo ukaongeza.

Gitau aliandika kuwa polisi wangemkamata kwanza wangemuitisha hongo ya Sh100, 000 ili asiuawe ama kushtakiwa lakini baadaye wamwandame na kisha kumuua.


Kero



Akithibitisha kisa hicho, Afisa Mkuu wa Polisi katika Wilaya ya Kigumo Bw John Katumo alisema Bw Gitau alikuwa kero kwa maafisa wa usalama kufuatia juhudi zake za kukusanya ushuru haramu kutoka kwa sekta ya Matatu haswa katika barabara ya Kaharate hadi Kangari.

“Tumekuwa tukimsaka lakini kwa bahati mbaya amejiua kabla ya tumpate.

Lakini nia yetu haikuwa kumuua, tulikuwa tu tumuonye arekebishe mienendo yake ya kuongoza vikundi vya kutoza magari ya uchukuzi na pia bodaboda ushuru haramu,” akasema.


Alisema amefurahia ujumbe ambao Gitau aliacha wa kuwahamasisha vijana watii sheria ili kujiokoa wenyewe akisema kuwa wafuasi wa makundi yote haramu hayana pa kujificha kwa sasa.

“Sheria itawaandama kwani mienendo yao inaathiri pakubwa utangamano na maendeleo katika jamii. Kazi yetu ni kuhakikisha maisha ya wananchi yanaendelea kwa mkondo ulio sawa bila ya kutatizwa na vizuizi vya ujambazi,” akasema.


SWAHILI HUB.COM
Na MWANGI MUIRURI
Imepakiwa - Wednesday, July 24  2013