Sunday 14 July 2013

MISS TANZANIA AMNYANYASA NA KUMTESA MAMA YAKE



Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mshiriki wa Miss Tanzania 2002, Samia Khan (26) anadaiwa kumfanyia vitendo vya kitumuwa mama yake mzazi ikiwa ni pamoja na kumpiga na kumfungia ndani bila kula.

Inadaiwa Samia mkazi wa Ungindoni, Kigamboni jijini Dar es Salaam, alifanya unyama huo kwa kipindi cha mwezi Juni mwaka huu kwa kushirikiana na mchumba wake mwenye uraia wa nchi ya Uingereza.

Akizungumza na NIPASHE Jumapili, mama mzazi wa Samia, Anitha Charles (39), mwenyeji wa Lushoto mkoani Tanga, alisema binti yake alimfungia ndani kama mfungwa, kumtukana na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali ya mwili kwa kipigo.

Akiwa ndani ya nyumba moja isiyokamilika ujenzi wake alipohifadhiwa kwa muda, alisema chanzo cha kufanyiwa
 unyama huo ni madai ya mtoto wake kuwa anamuibia mchumba wake pesa wakati wao wakiwa hawapo.

Alidai tangu afike jijini Dar es Salaam, maisha yake yamekuwa magumu kila siku baada ya binti yake huyo kumfanyisha kazi za kitumwa kwa kumlazimisha kufua nguo za ndani za mchumba wake pamoja na kusafisha mbwa 12 anaowafuga.


Chanzo    NIPASHE JUMAPILI
 Imeandikwa na MOSHI LUSONZO

0 comments: