Monday 8 July 2013

MAUAJI NA AJARI ZA TOKEA MKOANI MBEYA TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

 


[BARAKAEL MASAKI - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WILAYA YA MBEYA MJINI - MAUAJI

MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA USIKU HUKO MTAA WA MBATA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ODEN S/O MKUMBWA, MIAKA 60, MNDALI, MLINZI BINAFSI MKAZI WA NONDE ALIUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALI MBALI ZA MWILI WAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA KAZINI KATIKA LINDO AMBALO NI DUKA LA MADAWA MUHUMU [PHAMACY] LILILOPO ENEO HILO. MBINU ILIYOTUMIKA NI WATUHUMIWA KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA KATIKA LINDO NA KUMUUA KISHA KUVUNJA DUKA HILO LA DAWA MUHIMU NA KUIBA DAWA ZA AINA MBALIMBALI PAMOJA NA FEDHA TASLIMU TSHS 600,000/=. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.

WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO ILIMA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.654 BPX AINA YA TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA IMANI S/O MWAKILEMA,MIAKA 34,KYUSA, MKAZI WA KYELA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MAGE D/O NSUKEMO,MIAKA 59,KYUSA,MKULIMA ,MKAZI WA ILIMA NA KUMSABABISHIA KIFO CHAKE MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU KWA AJILI YA MATIBABU. CHANZO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA ILEJE - AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA VIFO
.

MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBEBE WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI T. 863 BXC AINA YA SANYA AITWAE OBADIA S/O MWAKIPESILE,MIAKA 36,KYUSA,MKAZI WA MBEBE PAMOJA NA ABIRIA WAKE FRED S/O FUMBIKA,MIAKA 23,MNDALI,FUNDI UJENZI MKAZI WA ISANGA MBEYA NA KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALINI YA WILAYA YA ILEJE. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI. ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.




Signed By,
[BARAKAEL MASAKI - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

0 comments: