MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Thursday 31 December 2015

Jeshi la Polisi limesema limeimarisha ulinzi katika mkesha wa mwaka mpya katika mikoa yote nchini.


Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha  mwaka mpya wa  2016, wananchi hutumia muda huo kwenda  katika nyumba za ibada ama kusherekea katika maeneo mbalimbali ya starehe, ambapo uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo  vinavyohatarisha usalama wa raia mali zao.

Jeshi la Polisi nchini,limejipanga vizuri katika mikoa yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kwamba vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza  hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mkesha wa mwaka mpya vinadhibitiwa. 
 
Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia,fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu. 
 
Aidha,Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara. Simu za polisi endapo mwananchi atakuwa na taarifa ni 111 au 112. 
 
 Pia,  Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo. 
 
Vilevile, wananchi kuacha tabia ya kuchoma matairi barabani pamoja na kupiga mafataki. Aidha, yeyote atakayefanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
 
Nawatakieni watanzania wote kheri ya mwaka mpya.
Imetolewa na:Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.         

Zaidi ya milioni 389 za miradi ya wananchi wilayani Mvomero zimetumika bila mpangilio.


Kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 389 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika kijiji cha Bunduki tarafa ya Mgeta wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro zimepotea bila kufanya kazi zilizokusudiwa zikiwemo fedha za mradi mkubwa wa maji safi,mradi wa umwagiliaji pamoja na  ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Bunduki.

Akifafanua ubadhilifu wa fedha uliofanyika wakati wa utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji uliogarimu zaidi ya milioni 251 mwenyekiti wa kijiji cha Bunduki Michael Segelo amesema kijiji chake hakikushirikishwa katika utekelezaji na baada ya mradi kukamilika mwezi Novemba mwaka huu hawakukabidhiwa na haujawahi kutoa maji. 
 
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunduki Bwana Prosper Mkunule amesema hatakubali kuona fedha za wananchi zinapotea bure na kwamba afuatilia hadi waliohusika na ubadhilifu huo watakapochukuliwa hatua. 
 
ITV imemtafuta aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero wakati miradi hiyo inafanyika ili kuzungumzia sakata hilo  Bwana Wallas Karia ambaye amesema yeye alisha hamia manispaa ya Bukoba huku jitihada za kumtafuta mhandisi wa maji wa wilaya ya Mvomero Bwana Gabriel Ngongi zikigonga mwamba baada ya simu yake kutopatikana na kwa wakati huo. 

Shirika la umeme nchini Tanesco limefanikiwa kuwanasa watu wanaoiba umeme Rukwa

 
Shirika la ugavi wa umeme Tanesco mkoani Rukwa,limefanikiwa kuwabaini zaidi ya wateja kumi na mbili wa shirika hilo wasiokuwa waaminifu, kufuatia msako mkali unaoendelea hivi sasa,wanaotumia umeme bila ya kuulipia kama inavyompasa kila mteja,kwa kujiunganishia umeme kwa njia za ujanja ujanja na kuzifanya mita zao zisishindwe kusoma umeme unaotumika kwa usahihi.

Afisa mahusiano wa shirika hilo la umeme la Tanesco kwa mkoa wa Rukwa Bw.Samweli Mandari,akiongea kwenye maeneo ya kizwite mjini Sumbawanga wakati zoezi la kuwasaka wateja wasiokuwa waaminifu, amesema baadhi ya mafundi umeme wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakila njama na wateja wa umeme,ili waweze kutumia umeme bila ya kulipia malipo sahihi,jambo ambalo linaliingizia shirika hilo hasara kubwa na wala halifai kufumbiwa macho.
 
Mmoja wa watuhumiwa ambaye ni mpangaji wa nyumba iliyokutwa na matatizo ya kujiunganishia umeme kwa njia isiyokuwa halali, katika mtaa wa mtumbuka maeneo ya Kizwite manispaa ya Sumbawanga Bi Elizabeth Pangipita, amejitetea kuwa yeye alikuwa hajui lolote linaloendelea kwa vile pamoja na mpangaji mwenziwe walikuwa wakichangia malipo ya umeme,na kumpatia mwenye nyumba aliyesema kuwa yupo safarini.

Kundi la Saiga lalamikiwa kwa kubomoa nyumba za wananchi Nyamongo.


Baadhi ya wakazi wa mji mdogo wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani Mara wameanza kuyakimbia makazi yao na wengine kulazimika kulala nje na familia zao nyakati za usiku, baada ya nyumba zao kadhaa kubomolewa na kundi la vijana wa Kikurya maarufu kama Saiga linalodaiwa kutekeleza vitendo vya uhalifu, vikiwemo vya uporaji wa mali na fedha kwa mwavuli wa polisi jamii.


ITV imefika katika eneo la Nyamongo na kushuhudia baadhi ya nyumba zinazodaiwa kubomolewa na kikundi hicho cha Saiga ambacho kilianzishwa kwa nia njema na jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime/Rorya katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu,yakiwemo matukio ya mauaji,unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi, lakini kwa hivi sasa kikundi hicho kimeacha majukumu yake ya msingi na kuamua kujichukulia sheria mkononi ambapo watuhumiwa wa uhalifu huo wanasemekana kutorokea nchi jirani ya Kenya.
 
Viongozi wa dini katika eneo hilo la North Mara wamelitaka jeshi la polisi kuacha kufumbia macho vitendo vya kihalifu vinavyohatarisha amani katika jamii kwa kisingizio cha mila kwani kundi hilo la Saiga haliko juu ya sheria na pia hakuna mila inayoruhusu kikundi cha watu kubomoa nyumba au duka la mtu na kuchukua samani za ndani, pesa au bidhaa nyingine yoyote. 
 
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya naibu kamishna Sweetbert Njewike,amekiri kuwepo kwa kikundi hicho ambacho pia kinahusishwa na mauaji ya wakazi wawili wa Nyamongo na kuhaidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuhusika na ubomoaji wa nyumba za wananchi kutokana na kujichukulia sheria mkononi.

chanzo Itv
 

Hicho ndiyo kilicho ikuta ndege ya AIR INDIA ikiwa na Abiria 171

Matukio yameendelea kuchukua headlines India.. ukiachia lile tukio la joto kali lililofanya watu kushindwa kuvumilia  na kukaa ndani ya maji wakihofia maisha yao huku wengine wakipoteza maisha kutokana na joto kali kuna hii nyingine imetokea huko.
Ndege ya Air India ambayo ilikua ikitoka Mumbai kuelekea London, Uingereza ililazimika kugeuza safari  ikiwa na abiria wake 171 na kurudi ilipotoka baada ya abiria kubaini kuwepo kwa panya ndani ya ndege hiyo.
Ingawa juhudi za kumpata panya huyo ziligonga mwamba  lakini  rubani  alilazimika kurudi Mumbai ili kuwatoa wasiwasi abiria zaidi ya 170 waliokuwa wakisafiri kwa kutumia ndege hiyo ya shirika la ndege la India.
Baada ya kutua abiria walilazimika kubadilishiwa ndege na kuanza safari upya ya kuelea London.
Unataka ku

MAZITO YAFICHUKA ,MBUNGE ALIZWA MAMILIONI KWA KUTAKA UWAZIRI HALAFU AKAUKOSA



WAZIRI na Naibu Waziri wake katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wameshindwa kufanikiwa kwenye juhudi zao za kushawishi wapate uwaziri katika Serikali ya Rais, Dk. John Magufuli, huku mmoja kati yao akitapeliwa shilingi milioni 40.
Viongozi hao wote walikuwamo katika wizara moja, kufuatia mabadiliko ya mwisho ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na Kikwete huku Raia Mwema likielezwa kwamba walitaraji nguvu ya ushawishi kupitia kwa “madalali” itafua dafu kwenye serikali ya Magufuli.


“Naibu Waziri wakati wa Kikwete ndiye aliyetapeliwa shilingi milioni 40. Huyu aliingia katika Baraza la Kikwete baada ya kushawishi kupitia kwa mmoja wa wake za kigogo mwandamizi serikalini. Mama huyo ndiye aliyemshawishi mumewe ambaye naye bila shaka alimshawishi Kikwete kwa sababu ni lazima washauriane katika uundaji wa baraza kutokana na nafasi zao za juu za uongozi nchini.
“Sasa alidhani awamu hii mambo yatakuwa hivyo hivyo, akakutana na ‘madalali’ ambao ni kweli wapo wengi na ninyi (gazeti la Raia Mwema) mlikwishawahi kuandika namna udalali ulivyokuwa ukifanywa na baadhi ya maofisa wa Ikulu hata katika kuweka miadi ya kumwona Rais.

“Jamaa (anamtaja jina) aliamini amekwishaweka mambo sawa, Magufuli alipotaja awamu ya kwanza ya Baraza lake hakuwamo na wala bosi wake wa zamani hakuwamo, wakajijengea matumaini kwamba akimalizia vile viporo vya wizara nne watakuwamo.

“Desemba 22, Naibu Waziri huyo wa zamani alipewa taarifa na madalali wake kwamba yumo kwenye orodha na kwa hiyo afike Dar es Salaam kwa kuwa siku inayofuata (Desemba 23) mawaziri watatajwa. Alisafiri usiku hadi Dar. Rais alipotoa taarifa ya mawaziri wake jioni ya Desemba 23 hakuwamo.

“Mwenzake (aliyekuwa waziri utawala wa Kikwete) alipanga kwenda kufanyiwa maombi Nigeria kwa Nabii T.B Joshua, sidhani kama atakwenda tena maana ilikuwa asafiri siku chake kabla ya Desemba 23, sijui nini kilimchelewesha hadi habari mbaya ikamkuta nchini kabla hajasafiri,” alieleza mtoa taarifa wetu na kusisitiza kwamba, Magufuli amepania kufuta udalali wa kusaka vyeo, na hata wahusika katika udalali huo wanajulikana kwake.

Waziri huyo anatokea mikoa ya Kanda ya Kati wakati Naibu wake akitokea mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Raia Mwema linashindwa kutaja majina ya mawaziri hao kwa kuwa juhudi za kuwapata kuzungumzia sakata hilo ziligonga mwamba, hata simu zao za mkononi hazikuweza kupatikana.

Viongozi hao wamewahi kuongoza wizara nyeti (jina linahifadhiwa) ambayo hata hivyo, katika utawala wa miaka 10 ba Kikwete ‘ilitema’ mawaziri kadhaa kutokana na kashfa mbalimbali, baadhi zikiwa ni zile zilizowahi kuibuliwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Magufuli, kwa mara ya kwanza alitangaza sehemu ya baraza lake la mawaziri Desemba 10, mwaka huu, baada ya kukaa kimya kwa takriban zaidi ya mwezi mmoja tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika baraza hilo, aliweka viporo vya mawaziri katika wizara nne, akitangaza mawaziri 14 tu kati ya Wizara 18 alizounda.

Wizara ambazo ziliwekwa viporo kwa maana ya kutopata mawaziri kutokana na kile Magufuli alichosema anaendelea kuwatafuta mawaziri husika, ni pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ambayo Naibu wake alimtangaza kuwa ni Edwin Ngonyani; Wizara ya Fedha na Mipango ambayo licha ya kuwa na waziri kiporo, Naibu wa Wizara hiyo alitajwa kuwa ni Dk. Ashantu Kijaji; Wizara ya Maliasili na Utalii haikupewa waziri kwa wakati huo ingawa Naibu wake alitajwa kuwa Mhandisi Ramo Makani.

Wizara nyingine iliyowekwa kiporo kwa wakati huo ni Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ambayo Naibu wake alitangazwa kuwa Mhandisi Stella Manyanya.

Baadaye, Desemba 23, Rais Magufuli alimalizia viporo hivyo ambapo alimteua Dk. Philip Mpango kuwa Mbunge na Waziri wa Fedha;  Profesa Makame Mbarawa kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; Profesa Jumanne Maghembe kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Dk. Joyce Ndalichako ambaye alimteua Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi baada ya kumteua kwanza kuwa mbunge. Katika orodha hiyo, vigogo hao wawili wa enzi za utawala wa Kikwete hawakuwapo.

chanzo:RaiaMwema

DIVA THE BOSS AMCHOKOZA JOKATE KWA PICHA HIZI










Angali Baby Madaha...Alivyo anguka Chooni na Kuvunjika Mguu.... ona hapaaaaaa'''''''''


MSANII wa filamu na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha hivi karibuni alipata majanga baada ya kuanguka chooni na kuvunjika mguu wa kulia, Amani lina taarifa zote.

Tukio hilo lilitokea nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar ambapo staa huyo alitoka kwenye matembezi yake usiku wa manane akiwa amepiga ‘mtungi’ wa kutosha.

Inadaiwa kuwa, alipofika kwake alihitaji kwenda bafuni kuoga. Hata hivyo, alianzia chooni kwanza na kutokana na miguu kukosa stamina kwa ‘ulabu’, alijikuta akiteleza na kudondoka chini kisha kuvunjika mguu huo.

Muonekano wa mguu huo uliovunjika.
Amani lilimsaka msnaii huyo ili kuzungumza naye kuhusu madai hayo ambapo alikiri kupata majanga.Baby Madaha alisema msala huo ulimfika majira ya saa 10 alfajiri (siku hakumbuki) akitoka kwenye kujirusha ambapo siku hiyo pombe zilimkoma kwa kufakamia kila aina.

Naamini kufakamia kwangu pombe nyingi ndiyo kuliniponza. Sijawahi kupata maumivu makali kama haya maana baada ya kudondoka chini nilijisikia sina nguvu wala sikuweza kusimama, nikalazimika kuukanyagia mguu wangu.

Ilipofika asubuhi nilijikaza kwenda Hospitali ya AAR iliyopo Kijitonyama (Dar) ambapo walinipiga X-Ray na kungundulika kuwa, mguu wa kulia ulivunjika, hivyo nikafungwa mhogo (P.O.P),” alisema Madaha.

Alisema kwa sasa (Jumanne iliyopita), anaendelea vizuri sana na anawashukuru madaktari wa AAR kwani awali yeye alijua mguu huo aliteguka tu na ungetengemaa muda wowote.

Da! Lakini yote maisha, leo tambarare, kesho mlima. Binadamu huwezi kuishi katika tambarare siku zote wala mlima siku zote. Najua hili hogo litatoka, nitadunda kama kawa,” alisema mrembo huyo.

Source:Global Publishers

Wednesday 30 December 2015

UMEYA KINONDONI, ILALA MVURUGANO

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salim Mwalimu  
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salim Mwalimu

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimeng’amua mbinu za CCM kutaka kuwatumia mawaziri walioteuliwa na Rais kuwa wabunge, kushiriki vikao vya madiwani vitakavyochagua mameya wa Manispaa za Kinondoni na Ilala ili kushinda viti hivyo.
Chama hicho kimemtaka Dk John Magufuli kuwatendea haki wakazi wa Dar es Salaam kwa kuaapishwa madiwani wa manispaa zote, ili waanze kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salim Mwalimu alisema: “Mpaka sasa madiwani hawatekelezi wajibu wao kutokana na kutokamilisha matakwa ya sheria.
Alisema CCM inaogopa kupoteza umeya wa jiji na manispaa hizo, hivyo inajiandaa kuwatumia mawaziri walioteuliwa na Rais kujiongezea kura

Lipumba Amtwika Zigo Dr Shein Mgogoro Zanzibar

 


Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kumaliza mgogoro wa Zanzibar.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mgogoro wa Zanzibar utamalizwa kwa Dk Shein kuiruhusu Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.

Alisema pamoja na mazungumzo yanayoendelea kati ya CUF na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Shein ndiye mwenye uwezo kuumaliza mgogoro huo.

“Mazungumzo yanaendelea na hatujui yatafika mwisho lini, lakini Dk Shein ndiye anayeweza kuifanya Zanzibar iwe na amani au vurugu, ninashauri aruhusu kutangazwa kwa matokeo,” alisema.

Alisema amani na utulivu uliopo Zanzibar wakati wananchi wakisubiri hatima ya mgogoro huo, haiwezi kuwa ya kudumu kwani ikiamuliwa uchaguzi urudiwe wapo ambao hawatakubali.

Profesa Lipumba alisema uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa huru na haki na hata watazamaji wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali walishangaa matokeo yake kufutwa.

Alisema wananchi wa Zanzibar walishapiga kura na kwamba wanachosubiri ni matokeo vinginevyo haki yao ya kidemokrasia itakuwa imechezewa.

Oktoba 28 mwaka huu, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta uchaguzi huo kwa kile alichosema kulikuwa na kasoro ndani ya tume yenyewe na kwenye vituo vya kupigia kura.

Profesa Lipumba alisema mgogoro huo ukiendelea, utakwamisha msaada wa Dola za Marekani 472.8 milioni uliokuwa utolewe na Shirika la Maendeleo ya Milenia (MCC) la Marekani.

Alisema Bodi ya MCC ilikutana Desemba 16 na kushindwa kupitisha msaada huo kwa Tanzania huku hoja kubwa ikiwa kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar.

Alisema miongoni mwa matumizi ya msaada huo ilikuwa kuunganisha wateja wapya 300,000 kupata umeme.

“Hapa tunategemea busara za Dk Shein kuumaliza mgogoro ili tupate msaada huo wenye masilahi ya Taifa au kuendelea na mgogoro na kuukosa msaada huo,” alisema.

Akizungumzia suala hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Magdalena Sakaya alisema huu ni muda mwafaka kwa Dk Shein kuweka masilahi ya Wazanzibari mbele.

Alisema atawekwa kwenye vitabu vya historia kama atafanya uamuzi wa kuruhusu kutangazwa kwa matokeo hata kama viongozi wenzake wa CCM hawatapenda uamuzi huo.

“Lakini vurugu zikitokea, Shein atalaumiwa jumuiya za kimataifa yeye mwenyewe na atashangaa viongozi wenzake wa CCM watakapojiweka pembeni,” alisema.

Kubenea Akana Kumtukana Dc Makonda


Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (44) amekana kumtukana Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda tarehe 14 Desemba 2015 walipokutana katika Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd. kilichopo eneo la External Mabibo kwa madhumuni ya kutatua mgogoro kati ya wafanyakazi na uongozi wa kiwanda hicho

Katika kesi inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Wakili wa Serikali mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa alimsomea mshtakiwa maelezo ya kesi hiyo ambapo baadhi  ya mashtakiwa aliyakana.

Akisomewa maelezo ya kesi, Saed Kubenea alikiri kuwa ni mbunge wa Ubungo na pia alikiri kuwa anamfahamu mlalamikaji katika kesi hiyo kuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda na kwamba ni kweli kuwa tarehe 14 Desemba 2015 alifika katika Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd kulikokuwa na mgomo wa wafanyakazi.

Hata hivyo, alipoelezwa kuwa anashtakiwa kwa kosa la kumtolea lugha chafu Makonda ambapo alimwita kuwa ni kibaka, mpumbavu, mjinga na cheo chake ni cha kupewa kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu; Saed Kubenea alikana.

Kufuatia Kubenea kukana mashitaka yanayomkabili, Hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo , Thomas Simba alisema mashahidi sita wa upande wa mashtaka wataanza kutoa ushahidi wao Januari 20 na 21, 2016 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Taasisi za Dini Zatajwa Kuhusika na Utoroshaji wa Makontena Bandarini



Mashirika ya dini ni miongoni mwa taasisi zilizotakiwa kuwasilisha nyaraka kwa ajili ya kuhakiki kama yalilipa ushuru wa bandari uliosababisha Serikali kupoteza Sh48 bilioni.

Uwapo wa taasisi hizo za kiimani kwenye sakata hilo ulibainishwa jana katika orodha ya iliyotangazwa jana na Mamlaka ya Bandari (TPA) ambayo ina kampuni na taasisi 40 zaidi ya orodha iliyotangazwa juzi yenye kampuni 243. Kwa tangazo la jana, kampuni na taasisi zinazotakiwa kuwasilisha nyaraka kuhusu malipo hayo sasa ni 283.

Tangazo la TPA lilitolewa jana likiwa na tarehe ya Desemba 24, linazitaka taasisi hizo ambazo ni Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki, Caritas Tanzania na nyingine 281 kwenda kuchukua barua zao kwa ajili ya uhakiki wa malipo ya ushuru huo yaliyofanyika kuanzia Julai 2014 hadi Aprili, 2015.

Taasisi nyingine maarufu zilizopo katika orodha hiyo ni klabu maarufu ya mchezo wa soka ya Azam Football, kampuni maarufu ya Toyota Tanzania Ltd na Bakhresa Food Products.

Juzi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alizihusisha baadhi ya taasisi hizo 283 na upitishaji wa makontena 11,884 na magari 2,019 kwenye bandari bila kulipia ushuru wa bandari.

 Kubainika kwa ukwepaji huo ushuru, kunafanya idadi ya makontena yaliyohusika katika suala hilo kufikia 14,664. Awali makontena 349 yaligundulika kupitishwa kinyemela baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufanya ziara bandarini na mengine 2,431 kubainika baadaye.

Mbarawa aliwataka mawakala wa forodha na kampuni hizo 283 zinazotuhumiwa katika utoaji wa makotena na magari bila kulipia ushuru kupeleka vielelezo vya uthibitisho ndani ya siku saba kuanzia juzi.

Msemaji wa CCT, Mchungaji John Kamoyo alisema watafanya kama lilivyoagiza kwenda kuchukua barua zao.

“Kama walivyoeleza sisi tutaenda kuchukua barua na kufahamu kilichopo ndani na tutafanya kama walivyoagiza,” alisema Kamoyo huku akikataa kuhusisha wito huo na suala lolote linalohusina na ukwepaji wa kodi.

Katibu mtendaji wa Caritas Tanzania, Laurent Masui alisema atashirikiana na mamlaka hiyo kutimiza agizo hilo.

“Ni kweli tunahusika na utoaji mizigo bandarini lakini kwa wateja mahususi kutoka mashirika ya kidini ambayo husamehewa baadhi ya kodi na ushuru. Lakini tozo nyingine huwa tunalipa na kwa kuwa tangazo lenyewe linaonekana ni la kiutawala, basi nitawatuma maofisa wangu haraka wafuatilie ili tujue kama tulizidisha ushuru au tulitoa pungufu,” alisema Nasui.    

Kamanda Suleiman Kova, Astaafu Rasmi Jeshi la Polisi Tanzania!

 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, Ametangaza asubuhi ya leo katika kipindi cha kumekucha cha ITV kwamba anastaafu rasmi kazi yake ya Upolisi.

Tunamtakia kila la heri huko aendako.

AZAM YAZIDI KUPAA LIGI KUU BARA BAADA YA KUICHAPA MTIBWA SUGAR KWA BAO LA 'JIONI'

Azam FC imezidi kupambana kwenda kileleni baada ya kuitwanga Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la Azam FC lilifungwa na nahodha wake, John Bocco katika dakika ya 86 kwa mkwaju wa penalti.

Hata hivyo, Mtibwa Sugar watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nyingi zaidi za kufunga.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kufikisha pointi 35 na kuendelea kubaki katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga.


Mtibwa Sugar inaendelea kubaki katika nafasi ya tatu ikiwa  na pointi 27.

PLUIJM KUTOA NAFASI KWA WASIOCHEZA WAKIPIGE KOMBE LA MAPINDUZI

Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm mpango wake mpya alionao sasa ni kujaribu kuwapa nafasi na kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo katika michuano ya Ligi Kuu Bara.

Lakini mkakati huo utaanza kutumika kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza rasmi Januari 2, mwakani huko visiwani ikiwemo kuendelea kuangalia zaidi kasi za wachezaji wapya waliosajiliwa kikosini humo hivi karibuni.

Pluijm amesema kuwa nia yake ni kushindana lakini pia itakuwa ni fursa nzuri kuwapa nafasi vijana wengine wakiwemo wale waliopandishwa hivi karibuni wakitokea kikosi cha timu ya vijana maarufu kama Yanga B.

“Tutakwenda kupambana kama ilivyo kawaida huwezi kusema kwamba utachukua ubingwa kama hutaweka nia ya kufanya vizuri kwenye michezo ya awali, hivyo tutatumia ushindi wa kila mchezo ili kufikia hapo tunapopataka.

“Lakini pia itakuwa fursa nzuri ya kuangalia vijana wengine ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kutosha kwenye ligi na michuano mingine nao kutumika na kuonyesha zaidi, taratibu kutakuwa na mchanganyiko lakini nia ni watu kupata nafasi pia.

“Kwenye kundi letu tupo na Azam, Mtibwa pia, tunatoka ligi moja lakini kwenye mashindano haitakiwi kuogopa kitu, tutakutana nao na nia yetu ni kushinda,” alisema Pluijm aliyeiongoza Yanga SC kutwaa ubingwa wao wa 25 msimu uliopita.

Kinondoni Moto: Uchunguzi Dhidi ya Mhandisi Mussa Natty wasuasua


Ni kama wahusika wametishwa na hatua ya wakinga-kifua wa Mhandisi Mussa Natty. Pamoja na kurejea Dar es Salaam, kutokea babati, kwa ajili ya uchunguzi dhidi yake kwa tuhuma zinazomkabili, hadi sasa Mamlaka husika zimeshindwa kuanza uchunguzi huo.

Mhandisi Mussa Natty alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kabla ya kuwa Mkurugenzi wa Mji wa Babati huko mkoani Manyara alikosimamishwa kazi kupisha uchunguzi. Anakabiliwa na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo ile maarufu ya kuuzwa kwa fukwe ya Coco.

Taarifa za uhakika zinaonesha kuwa Mhandisi Natty, pamoja na kuwa na nyaraka za kutosha zinazomsafisha, anaondolewa matatizoni na Wakurugenzi wawili waliomtangulia katika Manispaa ya Kinondoni ambao ndiyo hasa waliokuwepo wakati mambo anayotuhumiwa nayo Mhandisi Natty yakitendeka.

Kutokana na kuachwa kando kama washukiwa, Wakurugenzi hao wa zamani na waliomtangulia Mhandisi Natty wameonesha utayari wao 'kumtetea' Mhandisi Natty popote. Pia, Mbunge wa Ubungo na Diwani wa Kata ya Ubungo, Kubenea na Jacob, wameapa kuanika ukweli mambo yakianza kunoga.

Mamlaka zimetishika. Zimepunguza kasi. Zinajiuliza mara mbilimbili. Zinatafakari uwezekano wa kuanza upya kwa kuhusisha watu wapya!

By Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam/JF

Serikali Kupeleka Sh. 18.77 Bilioni kila Mwezi shule za Sekondari na Msingi, kugharamia Elimu



SERIKALI imepanga kupeleka Sh. 18.77 bilioni kila mwezi katika shule za sekondari na msingi kwa ajili ya kugharamia elimu ili kutekeleza dhana ya elimu bure kuanzia Januari, 2016.

Taarifa hiyo ilitolewa Mjini Dodoma jana na Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa elimu bure.

Alianisha fedha zitakazotolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia elimu ni pamoja na gharama za mitihani ya kidato cha nne ambazo zitatolewa moja kwa moja na Serikali katika Baraza la Mitihani (Necta).

“Serikali itatoa pia ruzuku ya uendeshaji wa shule Sh. 10,000 kwa shule za msingi na Sh. 25,000 kwa shule za sekondari kwa kila mwanafunzi kwa mwaka.

“Vilevile itatoa Sh. 1,500 kwa siku kwa mwanafunzi kwa shule za msingi na sekondari  kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi wanaokaa bweni,”amesema.

Simbachawene amesema pia Serikali itatoa fedha kwa ajili ya fidia ya ada Sh. 20,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya kutwa na Sh. 70,000 kwa mwanafunzi wa sekondari kwa mwaka.

Amesema fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule zitasaidia pia uendeshaji wa shule za hosteli ikiwemo gharama za chakula, mlinzi, mpishi, umeme na maji.

Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri husika kuhakikisha fedha hizo zinafika kwa wakati na zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa.

Simbachawene amesema majukumu ya wazazi pamoja na mambo mengine yatakuwa ni kununua sare za shule, vifaa vya kujifunzia, gharama za matibabu, nauli, gharama za chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa na  kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wa bweni.

“Natoa wito kwa viongozi wote wakiwemo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kusimamia utekelezaji wa elimu bila malipo,” amesema.

Aidha, Simbachawene aliziagiza halmashauri na mikoa ambayo haikufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba kujieleza sababu za kutofanya vizuri.

“Iwapo itathibitika kwamba kuna wahusika walizembea kutimiza majukumu yao wachukuliwe hatua zinazostahili.

“Nawaagiza pia wakurugezi mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kwamba ifikapo Februari 15 mwakani wawe wamekamilisha miundombinu ya shule ili wawewezeshe wanafunzi 12,647 waliosalia kujiunga na elimu ya sekondari wanaenda shule,” amesema.

Simbachawene pia alizitaka kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaosababisha wanafunzi kukatisha masomo kwa utoro na mimba pamoja na wale waliooa watoto wa kike.

‘’Tusifanye kazi kwa mazoea, tunatakiwa tuendane na kasi ya Rais John Magufuli ya kufanya kazi kuwasaidia wananchi hasa katika sekta ya elimu,’’ amesema.