Wednesday 27 August 2014

ALGERIA YASIMAMISHA SHUGHULI ZA SOKA


Algeria imesitisha shughuli za kandanda kwa kipindi kisichofahamika kufuatia kifo cha mchezaji kutoka Cameroon, Albert Ebosse aliyekufa baada ya kurushiwa kitu na mashabiki. 

Shirikisho la kandanda la Algeria limefikia uamuzi huo siku ya Jumapili. Ebosse, 24, aligongwa na kitu kichwani wakati akitoka uwanjani baada ya mechi kumalizika kati ya timu yake JS Kabylie iliyofungwa na USM Alger siku ya Jumamosi, jijini Tizi Ouzou. Mamlaka za Algeria awali zilikuwa zimeufungia uwanja wa Novemba Mosi 1954 lilipotokea tukio hilo.

 Amri hiyo sasa inajumuisha viwanja vyote nchini humo. Shirikisho hilo pia limesema litatoa dola 100,000 kwa familia ya Ebosse, kiasi ambacho angelipwa katika muda wa mkataba wake. Zaidi ya hilo, wachezaji wa JS Kablylie, kila mmoja atatoa mshahara wa mwezi mmoja.

0 comments: