Monday 18 August 2014

JUKWAA LA KATIBA LA PAMBA MOTO KUHUSU KATIBA MPYA



  

DODOMA     

JUKWAA la katiba nchini limeshauri,mchakato wa kuandika katiba mpya uahirishwe hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutokana na jukwaa hilo kudai kuwa yapo mambo mengi yanayokwamisha mchakato huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma   mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deus Kibamba,ameyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni mahudhurio hafifu ya wajumbe wa bunge hilo hivyo kushindwa kushirikiana vema katika kuandaa mchakato huo.

Amesema kuwa mbali na hilo kuwepo kwa michakato mingine mikubwa kama unadikishaji unaoendelea wa vitambulisho vya taifa ,uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya kielektroniki  na uchaguzi wa Serikali za mitaa haiwezi kwenda sambamba na mchakato wa katiba mpya bila kuathiri kiwango cha ushiriki wa wananchi na ubora wa katiba itakayopatikana.

Aidha Kibamba amefafanua kuwa utungaji wa katiba mpya unahitaji miaka ipatayo miwili tangu kupitishwa kwa katiba mpya hadi kukamilisha  uandaaji na upitishaji wa sheria zote takriban 50 zinazohitajika ili kusaidia utekelezaji wa katiba mpya .

Hata hivyo Kibamba ameongeza kuwa kitendo cha wajumbe kutoka kundi la UKAWA kugawanyika na hata baadhi ya wajumbe kutoka CCM kutofautiana kauli katika mchakato huu inaonesha kuwa taifa limeanza kugawanyika na utatuzi pekee ni kusitisha mchakato wa bunge maalumu la katiba.

0 comments: