Monday 11 August 2014

Rais wa Iraq hamtaki Nouri Maliki


  
Al Malik anasisitiza kuwa anataka kuongoza kwa muhula wa tatu
Rais wa Iraq Fuad Masoum amemtaka Kiongozi wa Kishia aliyeteuliwa na vyama vya kishia kuchukua wadhfa wa waziri mkuu katika bunge la taifa hilo kubuni serikali mpya.
Kiongozi huyo mpya ni naibu Spika wa Bunge Haider al-Abadi.
Kwa kumteua Abadi,vyama hivyo vinatoa changamoto kwa kaimu waziri mkuu Naouri Al Malik ambaye amesema wazi kwamba anawania kuliongoza taifa hilo kwa awamu ya tatu.
Hali ya taharuki imetanda katika mji wa Baghdad baada ya al maliki kutofautiana na Rais wa Iraq.
Hatua hiyo ya muungano wa vyama vya kishia ni pigo kwa bwana malik ambaye amekuwa akidai kuungwa mkono na makundi yote ya kishia nchini Iraq.
Bwana Malik ambaye anaonekana kama mtu anayewagawanya raia wa taifa hilo, amekuwa akizuia juhudi za kupata suluhu ya kisiasa katika nchi hiyo ambayo inakumbwa na tishio kutoka kwa wapiganaji wa Jihad katika maeneo yake ya kazkazini.
Wapiganaji wanaomuunga al Maliki wameonekana katika mitaa kadhaa ya Baghdad
Malik amesisitiza kuliongoza taifa hilo kwa awamu ya tatu,licha ya pingamizi kutoka kwa makundi kadhaa nchini Iraq na ushauri wa kiongozi mkuu wa dini, Ali al-Sistani ili kubadilisha uongozi.
Kuna matumaini kuwa uteuzi huo mpya utalisadia taifa hilo kukabiliana na changamoto zake.

0 comments: