Wednesday 23 July 2014

BOJAN KRKIC AMKIMBIA SUAREZ BARCELONA, AKIMBILIA STOKE CITY KWA MIAKA MINNE

KOCHA wa Stoke City, Mark Hughes amekamilisha usajili wa mchezaji wa tano kuelekea msimu ujao, baada ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona, Bojan Krkic kwa mkataba wa miaka minne.
Bojan – ambaye awali alimvutia Hughes alipokuwa kocha wa Manchester City miaka mitano iliyopita– amekamilisha uhamisho wake kutua The Potteries leo mchana baada ya kukiri kusajiliwa kwa Luis Suarez Nou Camp kunazidi kupunguza nafasi yake ya kucheza La Liga.
Taarifa katika akaunti ya Twitter ya Stoke imesema: 'HolaBojan Stoke City inayo furaha kuthibitisha usajili @BoKrkic kutoka @FCBarcelona kwa mkataba wa miaka 4'.

Krkic (kulia) angesotea namba kama angebaki Barcelona 

0 comments: