Saturday 26 July 2014

MARCIO MAXIMO AHITAJI KUONA UWEZO WA KHAMIS KIIZA NA EMMANUEL OKWI



Maximo ahitaji kuona uwezo Kiiza na Okwi.
Baada ya Maximo kumsajili Jaja Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakiumiza kichwa kutaka kujua mchezaji gani kati ya Kiiza na Okwi atakatwa kwenye usajili

 
KOCHA wa Yanga Marcio Maximo amesema pamoja na kumpa mkataba wa miaka miwili Mshambuliaji Geilson Santana Santos ‘Jaja’lakini bado anahitaji kuona uwezo wa washambuliaji wawili raia wa Uganda Hamisi Kiiza na Emmanueli Okwi.
Maximo ameiambia Goal kwamba anataka kuwa na timu imara itakayohitaji wa wachezaji wote na siyo mchezaji mmoja mmoja kama zilivyo baadhi ya timu nyingine ambazo ikitokea mchezaji huyo anaumwa zinashindwa kufanya vizuri.
“Nalazimika kuwaona mazoezini Okwi na Kiiza ndiyo nitakuwa na jibu la kusema lakini kwa sasa bado ni mapema mno kusema nitampunguza nani kwa sababu hata katika rekodi za klabu naona wachezaji hawa wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu ukitoa usumbufu ambao inasemekana wanao,”alisema Maximo.


Baada ya Maximo kumsajili Jaja Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakiumiza kichwa kutaka kujua mchezaji gani kati ya Kiiza na Okwi atakatwa kwenye usajili wa msimu ujao huku kila mtu akiwa na mapendekezo yake.
Chanzo:Goal.com

0 comments: