Saturday 26 July 2014

ASERNE WENGER AFICHUA SIRI YA KUOKOA KIWANGO CHA AARON RAMSEY


Wenger reveals pep talk that revived Ramsey’s career

BOSI wa Asernal, Mfaransa, Aserne Wenger amefichua siri kuwa alikaa kwa kirefu na Aaron Ramsey kwa lengo la kuzungumza naye ili kunusuru kiwango cha nyota huyo wa Wales.

Majeruhi ya mfululizo iliathiri sana kiwango cha nyota huyo mwenye miaka 23, lakini alionekana kuwa msaada katika klabu ya Asernal wakati wa harakati zake za kumaliza ukame wa miaka 9 bila kikombe msimu uliopita.

Baada ya kukaa chini na kocha wake, Ramsey aliibuka tena na kuwa moja ya wachezaji nyota wa ligi kuu msimu uliopita, akifunga mabao 16 na kuisadia Asernal kutwaa kombe la FA.

“Nilikaa chini na Aaron na nilimwambia, ‘Sidhani kama watu hawakupendi, lakini hawapendi mchezo wako kwa wakati huu’, Mfaransa huyo alieleza wakati wa ziara yao ya maandalizi ya kabla ya msimu nchini marekani.

“Alitakiwa kurejea katika mchezo wake….halafu ulimuona mchezaji tofauti, kwasababu ana akili, na baada ya kutoka katika mazungumzo, nilijua kijana ataweza kurudi  upya”.


Ramsey alianza katika ushindi wa Asernal wa mabao 2-0 dhidi ya Boreham Wood, ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa kirafiki wakati huu wa maandalizi ya kabla ya msimu, na anatarajiwa kucheza dhidi ya New York Red Bulls siku leo jioni.

0 comments: