Saturday, 19 July 2014

AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207
MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA, JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 26 – 30 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.320 AQV AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE OMARY KASYUPA (46) MKAZI WA KIWILA – TUKUYU.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.07.2014 MAJIRA YA SAA 07:30 ASUBUHI KATIKA ENEO LA MWISHO WA MJI, KATA YA BAGAMOYO, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARANI HASA WATEMBEA KWA MIGUU KUVUKA KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO NA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA.
TAARIFA ZA MISAKO:
MSAKO WA KWANZA:
WATU WAWILI WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA UPENDO WILAYA YA CHUNYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. KURUSUMU KALUKALA (36) NA 2. MATILDA TUSKER (24) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA 90.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.07.2014 MAJIRA YA SAA 07:10 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MALANGALI, KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAPIKAJI/WATENGENEZAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO.
KATIKA MSAKO WA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA KITONGOJI CHA MACHINJIONI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MELLAMA RICHARD (52) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA SABA (07).
MTUHUMIWA ALIKAMATWAMNAMO TAREHE 18.07.2014 MAJIRA YA SAA 11:48 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MACHINJIONI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MTENGENEZAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA POMBE HIYO ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments: