Thursday 24 July 2014

AZAM FC YAITANDIKA RUVU SHOOTING 1-0 MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI


MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc leo asubuhi wamecheza  mechi ya kujipima uwezo dhidi ya Ruvu Shooting katika dimba la Azam Complex, Mbande, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Hadi dakika 90 zinamalizika, Azam fc walikuwa mbele kwa bao moja lililofungwa kipindi cha pili na kinda wake, Bryson Raphael.

Mechi hiyo ilitumika na makocha wa timu zote, Joseph Marius Omog wa Azam na Tom Alex Olaba Ruvu Shooting ili kuangalia kama wachezaji wao wanashika mafundisho.

0 comments: