SIMBA
SC itacheza na Ismailia ya Misri au Zesco United ya Zambia katika
tamasha maalum la klabu hiyo la kila mwaka, maarufu kama Simba Day
Agosti 9, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema leo katika
mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi
kwamba, kipaumbele cha kwanza ni Ismailia na iwapo itashindikana Zesco
itachukua nafasi.
Kaburu
amesema mchakato wa usajili unaendelea na jana mchezaji wa Burundi
amewasili wakati kesho Kamati ya Usajili itakutana naye kwa mazungumzo.
|
Simba SC inaendelea na mazoezi Dar es Salaam |
Beki
Mrundi, Kaze Gilbert ameomba aandikiwe barua ya ruhusa ya kwenda
kujiunga na klabu yake ya zamani, Vital’O, wakati beki chipukizi Hassan
Hatibu anatakiwa na Kagera Sugar.
Kaburu
amesema wamekubali maombi yote la Kaze na Kagera Sugar na
watawaidhinishia wachezaji hao, ambao kwa sasa hawana nafasi kwenye
kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi.
Amesema klabu hiyo pia imeridhia mshambuliaji wake Betram Mombeki kujiunga na JKT Ruvu, maana yake imefuta mkataba wake.
Kuhusu
kocha wa timu hiyo, Mcroatia Zdravko Logarusic aliyemaliza Mkataba
wake, Kaburu amesema kwamba wanatarajia kumpa Mkataba mpya wiki ijayo
kabla ya timu kwenda kambini visiwani Zanzibar kujiandaa na msimu mpya.
Simba
SC pia imetangaza nafasi za kazi kwa Katibu, Msaidizi wake na Ofisa
Habari na Kaburu ameomba watu watume maombi ili kuiwezesha klabu kufanya
uteuzi. Katibu wa Simba SC kwa sasa ni Ezekiel Kamwaga, wakati Ofisa
Habari ni Asha Muhaji.
Na Nagma Khalid, DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment