Wednesday 23 July 2014

JAMES RODRIGUEZ ATAMBULISHWA RASIM LEO RAIS PEREZ KUVAA JEZI NAMBA 10

REAL Madrid wametangaza rasmi kumsajili mfungaji bora wa kombe la dunia,  James Rodriguez kwa dau la paundi milioni 60 kutoka klabu ya Monaco baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Nyoya huyo wa kimataifa wa Colombia amekubali kusaini mkataba wa miaka 6 na Real Madrid baada ya kuchukuliwa vipimo vya afya jana asubuhi kabla ya kutangazwa mbele ya mashabiki ndani ya dimba la Santiago Bernabeu.

Rais wa Madrid,  Florentino Perez alimkaribisha mshambuliaji huyo na kumfananisha na gwiji wa klabu ,Alfredo Di Stefano aliyejiunga na Real kutokea Colombia.
Signed: James Rodriguez was unveiled as a Real Madrid player on Tuesday at the Santiago Bernabeu
Amesaini: James Rodriguez alitangazwa jana jioni kuwa mchezaji rasmi wa Real Madrid ndani ya uwanja wa  Santiago Bernabeu
Hands in the air: Rodriguez acknowledges the crowd at the Bernabeu as he is unveiled as a Real player
Mikono juu: Rodriguez akiwakubali mashabiki waliofurika dimba la Bernabeu wakati akitangazwa kama mchezaji wa  Real 
Arrival: Rodriguez poses with a ball during his presentation on the pitch at the Santiago Bernabeu
Ametua: Rodriguez akipozi katika picha wakati akitambulishwa Santiago Bernabeu
All smiles: Real Madrid president Florentino Perez (left), Rodriguez (right) and his wife Daniela at presentation
Tabasamu: Rais wa Real Madrid , Florentino Perez (kushoto), Rodriguez (kulia) na mke wake Daniela wakati wa utambulisho.Skills: Rodriguez showed played up to the crowd with some flicks and tricks out on the pitch
Muda wa maufundi ukawadia ambapo Rodriguez alionesha uwezo wa juu.
Control: Rodriguez put on an impressive display for the Madrid fans at the Bernabeu 
Control: Rodriguez put on an impressive display for the Madrid fans at the Bernabeu
 Rodriguez aliwavutia mashabiki Bernabeu
Taking it down: Rodriguez wore some pink and blue boots during his unveiling
Mambo ya Rodriguez, mfungaiji bora wa kombe la dunia.
Love? Rodriguez kisses the badge on the Real Madrid kit during his presentation at the Bernabeu
Mpenzi? Rodriguez akibusu nembo ya klabu kwenye jezi ya ya Real Madrid 
Squad number: Rodriguez will wear the '10' jersey at Madrid next season
 Rodriguez atavaa jezi namba 10 msimu ujao

JAMES RODRIGUEZ ATAIMUDU ADA YAKE YA UHAMISHO REAL MADRID?

All smiles: Real Madrid president Florentino Perez (left), Rodriguez (right) and his wife Daniela at presentation
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Mtandao

 
KULIKUWA na maswali mengi zaidi kuliko majibu kufuatia James Rodriguez kujiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 80 sawa na paundi milioni 60 kutokea klabu ya Manaco.
Wapi Mkolombia huyo atacheza?  anastahili ada kama hiyo ya uhamisho?, kweli Real Madrid inamhitaji yeye?
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez hana wasiwasi. Kiwango kikubwa alichoonesha katika fainali za kombe la dunia akiwa na taifa lake ndio sababu ya Real kumsajili majira haya ya kiangazi.
Usajili huo umekuwa mkubwa zaidi ya Toni Kroos aliyesaini mkataba wa miaka sita na mabingwa hao wa Ulaya wiki iliyopita.
Licha ya kipaji alichonacho Rodriguez, mashabiki wa Real Madrid wamebaki wakishangaa kama kweli mchezaji huyo mpya atakayevalia jezi namba 10 atang’ara na klabu kama alivyofanya Brazil akiwa na Colombia.
Mchezaji huyo wa zamani wa Porto alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa kombe la dunia kwa kufunga magoli sita na kuiongoza Colombia mpaka hatua ya robo fainali.
Pia aling’ara akiwa na klabu yake ya Monaco katika michuano ya Ligue 1 msimu uliopita, lakini amekuja katika macho ya watu wengi zaidi majira haya ya kiangazi.
Wakati Kroos akiwasili kwa dau linaloingia mara tatu kwa lile la Rodriguez baada ya kushinda kombe la dunia, nyota huyo kijana ameingia katika orodha ya wachezaji ghali zaidi duniani akishika nafasi ya nne baada ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.
Kuwa na kipaji, hakuna wasiwasi, lakini kuna vitu vingi vya kuthibitisha.
Je, mchezaji huyo wa Monaco na Porto anaweza kuonesha vitu vyake Real Madrid mbele ya wachezaji wengi nyota?
Kitu cha kwanza: Mchezaji huyu mwenye miaka 23 ana kipaji. Kucheza nyuma ya mshambuliaji akiwa na Colombia nchini Brazil kulimfanya aonesha uwezo mkubwa akifunga bao zuri lililojadiliwa kuwa miongoni mwa mabao bora.
Skills: Rodriguez showed played up to the crowd with some flicks and tricks out on the pitch
Alionekana kuwa mtulivu kwenye michuano hii mikubwa zaidi duniani. Pia alipiga pasi za mwisho za mabao 12 katika ligi ya Ufaransa msimu uliopita  na alifunga mabao 9 akiwa na Monaco na alitajwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo.
Madrid wamemsajili mchezaji anayeweza kwenda katika kiwango cha juu zaidi.
Atacheza wapi Bernabeu? Wakati huu Kroos akiwa amejiunga na mabingwa hao wa ulaya. Angel di Maria na Sami Khedira wanaweza kuondoka klabuni hapo majira haya ya kiangazi, lakini bado swali linabaki kama Mcolombia huyo ataweza kuingia katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid.
Siasa zinaweza kutawala hili. Baada ya Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, Rodriguez atakuwa mchezaji ghali zaidi kwenye kikosi cha Real Madrid na Perez hatapenda kuona fedha kubwa kiasi hicho zinakaa benchi.
Kocha Carlo Ancelotti atalamizika kumchezesha mchezaji huyo hata kama anapenda au hapendi.
Love? Rodriguez kisses the badge on the Real Madrid kit during his presentation at the Bernabeu
Lakini  katika jicho la ufundi, Rodriguez hawezi kuanza katika kikosi cha kwanza kwa wakati wote.
Nyota huyo anapenda kucheza nyuma ya mshambuliaji, kwa mazingira hayo atakuwa Karim Benzema.
Lakini Cristiano Ronaldo na Garthe Bale wote huwa wanaanza, kuongezeka kwa Rodriguez kutamfanya Ancelotti aanzishe kikosi kitakachoshambulia zaidi. Huo ndio utamaduni wa Real Madrid, wengine wanasema kuwa na usawa kikosini sio suala muhimu.
Viungo wawili wa kati wataachwa kulinda safu ya ulinzi na kuunganisha safu ya ushambuliaji, lakini msimu uliopita, Real Madrid walikuwa wanayumba katika safu ya kiungo wanapocheza na timu kubwa. Tatizo yawezekana lilikuwa katika mfumo wa kwanza wa 4-2-3-1 uliokuwa unawapa nafasi wachezaji wote nyota.
Badala yake, mfumo wa 4-3-3 unaoogopwa zaidi wa `BBC`, Bale, Benzema na Cristiano Ronaldo utatumika tena, katikati watakuwa watatu, Kroos, Xabi Alonso na Luka Modrid , huku Rodriguez akiwa benchi, na unaonekana kukamilika.
Squad number: Rodriguez will wear the '10' jersey at Madrid next season
Wachezaji wote watatu wa katikati wanaweza kusaidia ulinzi na wanaweza kucheza kama viungo wa ulinzi. Kuwapanga wawili na kumuingiza Rodriguez kutaifanya timu ishambulie zaidi na haitakuwa busara kwa safu ya ulinzi.
Kwahiyo Rodriguez atafanya nini? Ancelotti alionekana kumuongeza Isco katika safu ya kiungo cha kati msimu uliopita. Kitendo kilichomfanya nyota huyo ashindwe kuonekana vizuri na kuachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.
Rodriguez anaweza kucheza vizuri nafasi hiyo na itakuwa nzuri zaidi baada ya Alvaro Morata  kuondoka na kujiunga na Juventus majira haya ya kiangazi. Kuna uwezekano wa kucheza na Ancelotti ataweza kumtumia.
Ada kubwa ya uhamisho haijamsaidia Rodriguez; ada kubwa kazi hizo hazifanyi kazi. Kunakuwa na presha kubwa kwa wachezaji wa aina hiyo Real Madrid, lakini ada hiyo ambayo ni ya nne kwa ukubwa katika historia ya uhamisho wa wachezaji itaongeza majukumu zaidi kwenye mabega ya mshambuliaji huyo.
Haijulikani kama atamudu ada yake au atashindwa kama walivyoshindwa wachezaji wenzake Isco na Asier Illarramendi, waliowasili Bernabeu kwa ada kubwa msimu uliopita, lakini walishindwa kutamba na kubaki kukalia benchi.

Mambo yanavyoonekana, Usajili wa Rodriguez unaonekana kuwa wa kujifurahisha na sio lazima. Ni juu yake kuwathibitishia watu uwezo wake. 

0 comments: