Monday, 21 July 2014

MKUU WA SHULE AKANUSHA UVUMI WA KUVULIKA NA KUJAA KWA VYOO VYA SHULE YAKE



mkuu wa shule ya msingi ya iwambi bwana ROPHIN B MARYA akiwa katika kazi yake ya kila siku

mkuu wa shule ya iwambe na mwalimu mwenzake

muonekano wa nje wa vya shule ya msigi iwambi


 Hivi ndio vyooo vilinavyo sadikiwa kuwa vimajaaa na kufulika


 Muonekano wa shule ya msingi iwambi

Hawa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi iwambi


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi iwambe iliyopo mkoa wa mbeya  bwana ROPHIN B MARYA  akanusha uvumi ambao umejitokeza kwamba vyoo vya shule yake vimefulika na avifai kwa matumizi ya wanafunzi  wa shule hiyo ,hayo ameyasema baada ya vyombo vya habari kupata taarifa za kujaa kwa  vyoo na avifai kwa matumiza ya wanafunzi  nakutaka ajibu tuhuma hizo

Mwalimu Marya amesema tatizo hilo llikuwepo zamani lakini sio kwasasa kwa kuwa    shule ina matundu 14 wasichana wanatumia matundu 7  wavulana nao wana tumia matundu 7  pia ameongeza kuwa awali walikuwa wakitumia  7 tu  kwa matumiza wanafunzi  zaidi ya 1400  hali ambayo ilikuwa nihatari kwa afya za wanafunzi nametaja  sababu ya kutumia vyoo vichache amesema  tatizo  ilikuwa shule kukosa  maji  yakutoshaaa  na vingine bomokabomoka

Akiongeo kwa msisitizo amesema kwa sasa  wameweka maji kwenye vyoo vyote  vipya na ambovyo vilikuwa havitumiki baada ya kuwepo kwa maji ndio vikaanza kutumika rasmi  matundu 14  hivyo   hajaona kwamba kuna Msongamano wa wanafunzi kushindwa kutumia  vyoo hivyo kwa kuwa kwa sasa wanatumia  kama kawaida, ila meiomba kamati ya shule hiyo napamoja na serikali kujenga vyoo vingine  kwa kuwa idadi ya wanafunzi ni wengi kulingnisha na vyoo vilivyopo hivi sasa

Akizungumzia Suala la watoto kula chakula shuleni hapo amesema waliitisha kikao cha wazazi na kuwaeleza lakini wazazi walipinga kabisa suala hilo na baadaye tulishindwa kuendesha zoezi hilo na wazazi hao walidai kuwa seriikali ndio iwe ya kwanza kutoa msaada na kutekelezaji wa swala hilo  ndipo wao watafata kwa kuwa serikali  ndio imetaka zoezi hilo  lifanyike


0 comments: