Monday, 21 July 2014

NGUVU YA WANANCHI YAWEZESHA KUTENENEZA BARABARA JUU YA MLIMA



         

Baadhi ya wananchi wakitoka katika kazi ya maendeleo ya utengenezaji wa barabara

Huu ndio muonekano wa barabara iliyopo juuu ya mlima  kati ya kata ya Iziwa na na itende


Ni wananchi wa kata ya itende na maziwa wakiwa katika harakati za kutengeneza barabara


  
Wananchi wa kata ya  Itende  mtaa wa  gombe na Iziwa  mkoani mbeya wameamua kutengeneza Barabara  Inayo unganisha kata hizo   mbili kwa kurahisha mawasiliano baina yao na kukuza undugu.kwa awali barabara hiyo ilikuwa hapitiki kwa kuwa ipo mlimani
Mwenyekiti wa mtaa wa Gombe Bahati Mwasote  ameleza kuwa kutokana na kukosa njia ya kudumu waliamua kukutana na kuweka mikakati ya kutengeneza Barabara hiyo ili kuwa makubaliano ya kata zote mbili  na kuanza kutengeneza Barabara hiyo  nakwa  kupanga rataba ya kila alhamisi  ifanyike utengenezaji wa barabara hiyo   ili kuwezesha wananchi kufanya shughuli zao kwa kutu mia barabara hiyo .
Kwa upande wake mwenyekti  wa mtaa wa Iziwa Ndg.David Ndalama  amesema kuwa wametengza barabara hiyo wenyewe kwa kumia mikono na gharama zao wenyewe bila msaada wowote bila kutoka serikalini hivyo wanayomba serikali na mashirika kutoa msaada  wakutengeza barabara hiyo kwa kuwa wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo vifaa duni, wa  ukosefu wachakula, hali ambayo hupelekea wananchi kukata tamaa  ukizangati barabara ipo juu  ya mlima ‘’ alisema  mwenyekiti huyo’’
Baadhi ya wananchi  walio shiriki maendeleo ya utengenezaji wa  barabara hiyo  wamesema wame acha  mambo mengi kama  biashara,kulea familia kwa kuwa  lengo lao kubwa  ili kuwa nikutengena barabara na    sasa wameweza kupasua barabara kwenye mlima hata kuzuia majanga ya moto kwenda upande mwingine  
  wananchi hao wameomba   serikali kuungwa mkono kwa kile wanacho kifanya kwa kuwa  wanacho kifanya sio wao tu watakao tumia barabara hiyo ila ni ya watu wote watokao sehemu mbalimbali ,hivyo serikali itazame wananchi wa kata hiyo walicho kifanya
                                                

Habari Na: Abdul Marwa MBEYA                    

0 comments: