Wednesday 23 July 2014

TETESI ZA USAJIL : MONACO YAINGIA VITANI NA REAL MADRID KUISAKA SAINI YA FERNANDO TORRES



European interest: Monaco and Atletico Madrid are keen on signing Fernando Torres
 Monaco na Atletico Madrid wanaitaka saini ya Fernando Torres.

Imechapishwa Julai 23, 2014, saa 6:00 asubuhi

KLABU ya Monaco imeingia katika vita na Atletico Madrid kuiwinda saini ya mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye miaka 30 anahitaji kutafuta timu ya kupata nafasi ya kucheza, lakini Chelsea watasikiliza ofa nzuri zaidi.
True blue: Torres may be reluctant to leave Chelsea following the arrival of Cesc Fabregas
Bluu ya kweli: Torres anaweza kugoma kuondoka Chelsea baada ya kuwasili kwa Cesc Fabregas

Atletico Madrid wanavutiwa kumrudisha nahodha huyo wa zamani wa Vicente Calderon baada ya kumuuza nyota wake  Diego Costa katika klabu ya sasa ya Torres ya Chelsea.

Chelsea wapo tayari kumuuza Torres kama ofa ya paundi milioni 20 itapatikana.
Msimu ujao, Jose Mourinho anataka kumtumia mshambuliaji mmoja tu ambapo Diego Costa ndiye atakuwa mshambuliaji namba moja.
Nafasi ya Torres itafifia zaidi kama Didier Drogba atarudi London Magharibi.
Summer signing: Diego Costa could be seen as a replacement for Torres
Jembe jipya:  Diego Costa atabadili nafasi ya Torres

0 comments: