Tuesday 22 July 2014

RAIS JOSEPH KABILA AALIKWA KATIKA HARAMBEE YA KUJENZI WA MAABARA YA SHULE YA SECONDARY SANGU

Wakwanza kushoto ni mkuu wa sule ya sekondari sangu bwana aANDENGWEZYE BUKUKU wapili  ni katibu wa umoja wa wazazi Tanzania  wilaya ya mbeya  bwana   JUMA MNG'OMBE  na wa tatu ni mkuu msaidizi wa kwanza  wa sangu sekondari  bwana GWANDGEH SOPHYLLIN

Muonekano wa shule ya sekondary sangu

Mkuu wa sule ya sekondari sangu bwana  ANDENGWEZYE BUKUKU wapili  ni katibu wa umoja wa wazazi Tanzania  wilaya ya mbeya  bwana   JUMA MNG'OMBE  walipokuwa wakiongea na vyombo vya habari


Mkuu wa sule ya sekondari sangu bwana  ANDENGWEZYE BUKUKU


 muonekano wa wanafunzi wakiwa darasani baada ya kutembelewa na vyombo vya habari

wanafunzi wakiwa darasani baada ya kutembelewa na vyombo vya habari


Shule ya sekondari sangu iliyopo mkoani mbeya  ambayo ipo chini ya umoja wa wazazi  Tanzania  jumuiya ya  ccm imeazimia kufanya harambee ya ujenzi wa maabara ya kisasa yatakayo fanyika katika ukumbi wa mkapa tarehe 14 mwezi wa nane,hayo yamesemwa na uongozi wa shule hiyo kwa kupitia mkuu wa shule ANDENGWIZYE BUKUKU ,
Alipo kuwa akizungu mza na vyombo vya habari  ofisini kwake ,ambapo amesema kuwa malengo ya kuandaa harambee hiyo ni kujenga maabara ya kisasa ambayo itawezesha wanafunzi wanao soma masomo ya sayansi hususani fizikia ,balogia na kemia iliwaeze kupata elimu bora ya sayansi  kwa ufanisi zaidi kwa kuwa kwasasa wana uhaba wa maabaara.


Bukuku amesema amewaalika baadhi wanafunzi  mbalimabili  waliwahi kusoma katika shule hiyo miongoni mwao ni rais wa jumuhuri ya demokrisia ya kongo(DRC) Mh joseph kabila ambaye aliwahikusoma hapo miaka kadhaa iliyopita,ameongeza kuwa uongozi wa shule hiyo umeamuakumwandikia barua ya mwaliko kupitaia ubarozi wa Tanzania kuhusu halambeee hiyo


Mbali na kiongozi huyo  mkuu huyo wa shule amewata baadhi ya wanafuzi wengine walio wahi kusoma hapo ni kama vile mbunge wa singda mjini MOHAMED DEWJI,aliyekuwa waziri wa mabo ya ndani na mbunge wa songea mjini EMANUEL NCHIMBI alikuwa mbunge wa mbeya mjini na hivi sasa ni mkuu wa wilaya ya kahama MH BENSON MPESYA na msanii maarufu Tanzania AMBYENE YESAYA (A .y)


Kwa upande wake katibu wa umoja wa wazazi Tanzania wilaya  ya mbeya  bwana  JUMA  MNGO’MBE amesma kuwa  ili kukakamilisha  ujezi wa maabaara wana hitaji jumla ya milioni miamoja  sitini  na moja  ( milioni  161) hivyo ame waomba wadau  mbalimbali iki wemo  tasisi za kifedha na wafanya bishara kujitokeza katika harambe hii ili kuwezesha elimu ya Tanzania kuwa ya ufanisi zaidi,na katika harambe yiyo mgeni   anatarajiwa kuwa Naibu waziri wa fedha Mh  ADAM KIGODA MALIMA  katibu huyo ameotoa namba  ya akaunti ya benki kwa wale wanao unga mkono harambee hii kwa kuchangia  kupitia  akunti namba CRDB 01j1065276501



Na A bdul  Marwa

kwa  Yule  anependa kujua zaidi ya hambee hii apige namba ya mkuu wa shule 0764600414

0 comments: