HOME »
» HAYA NDIYO MAMBO YA MINZIRO, NI BURUDANI YA ZIADA ZAIDI YA DAKIKA 90 ZA MCHEZO UWANJANI
MAKOCHA
wana vitimbi vyao wanapokuwa wanaongoza timu zao- na mara nyingi ambao
husisimua ni wale, ambao huwa hawatulii kwenye viti vyao wakati wa
mechi, wakiwapigia kelele wachezaji wao.
Hawa
huwa hawachelewi hata kutukana waamuzi au wakati mwingine hata kuwavaa
na kuwashambulia- kwa sababu wana kile kitu kinaitwa munkari.
Walimu
wengine baada ya kumalizana na wachezaji wao vyumbani, wanapoingia
uwanjani huwaacha hadi baada ya kumalizika kwa ngwe ya kwanza azungumze
nao tena.
|
Hapa anasema nao; Cheza mpira, namna hiyoo |
|
Hapa anamshangaa refa; Wewe refaa wewee |
|
Yowe la nguvu, kutoka Chamazi Kariakoo walimsikia |
|
Hapa anashangaa, au; Ameweka pozi anaangalia mchezo |
Lakini
Freddy Felix Isaya Kataraiya Minziro ‘Majeshi’ hayuko hivyo. Anatoka
kuzungumza na wachezaji chumbani, lakini mchezo ukianza kuanzia dakika
ya kwanza hadi ya mwisho anawapia kelele.
Tena
si kelele tu, atanyoosha mikono, ataibadilisha sura yake, ataruka ruka,
atakwenda na kurudi kama mtu aliyesusa- lakini atainuka tena na hali
itaendelea kuwa hivyo hadi mwisho wa mchezo.
Kwa wachezaji wagumu kuelewa, mwalimu anayewafaa ni Minziro kwa sababu anawakumbusha majukumu na wajibu wao muda wote wa mchezo.
|
Kama amesusa, lakini bado yupo kazini |
|
Mishipa ya shingo inasaidia kazi koo kupiga kelele |
Lakini
kwa mashabiki, Minziro huwa burudani ya ziada zaidi ya ule mchezo
unaoendelea uwanjani kwa vitimbi vyake. Sauti yake nyembamba na kali
pekee ni burudani tosha anapowapigia kelele wachezaji wake. “Cheza
mpira, nini hiyooo, haifaai” Aaaa weweee refaa weweee,”. Ni raha tu.
Baada
ya kuwa kocha Msaidizi wa klabu yake ya zamani, Yanga SC kwa takriban
miaka minne, Minziro amerudi kuwa kocha Mkuu wa Ligi Kuu kupitia klabu
ya JKT Ruvu.
Wiki
iliyopita Minziro aliiongoza timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi
ya Azam FC Uwanja wa azam Complex, Chamazi, Dar es salaam ambao
alipoteza kwa mabao 2-1.
Siku
hiyo, beki huyo wa zamani wa Yanga na timu ya mkoa wa Dar es Salaam
‘Mzizima’ alipiga kelele mno na kufanya kila aina ya vitimbi alivyoweza
katika kufikisha ujumbe kwa wachezaji wake.
Ilisaidia,
mwanzoni ilionekana kama JKT ingepigwa nyingi, baada ya kukubali mabao
mawili ya haraka haraka, lakini baadaye timu hiyo ya Jeshi ka Kujenga
Taifa ikasimama imara na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi katika
mchezo ambao wangeweza kupata sare au hata kushinda. Hayo ndiyo mambo
Minziro, anapokuwa kazini hataki mzaha.
0 comments:
Post a Comment