Moja ya askari akiwa amebeba kichanga kwenye mfuko wa lambo
VITENDO vya kikatili dhidi
ya watoto mkoani Mbeya vimezidi kushika kasi licha ya serikali na mashirika mbalimbali
kukemea vitendo hivyo, kufuatia mwanamke mmoja asiyefahamika jina wala makazi
yake kudaiwa kutupa kichanga chooni baada
ya kuharibu ujauzito wake.
Tukio hilo limetokea juzi
majira ya saa 07;20 mtaa wa Simike kata
ya Mabatini jijini Mbeya ambapo kichanga hicho kinachokadiriwa kuwa na miezi
saba hadi tisa tumboni, kiligunduliwa na mmiliki wa choo hicho Andrew Janco alipokuwa
akioga.
Akizungumza na Mbeyagreennews blog Janco alisema kuwa alipomaliza kuoga alishangaa kuona maji hayapiti
kwenye bomba la choo chake ambacho ni cha maji ndipo alipochukua mti na kuanza
kusukuma huku akihisi kuwa ni nguo imezuia maji yasipite.
Hata hivyo alisema kuwa
baada ya kusukuma kwa muda mrefu alizunguka nyuma ya choo na kukikuta kichanga
hicho kikiwa kimekufa ndipo alipotoa taarifa kwa majirani.
‘’nilipomaliza kuoga
nikahoji kwa nini maji hayatoki nikajua mke wangu ametupa nguo nikasukuma mpaka
mwisho kwenye shimo na nilipozunguka nyuma ya choo nikakuta mtoto amekufa
nikatoa taarifa isingekuwa misumali niliyopigilia kuzuia bomba lisianguke
nisingetambua kama kuna mtoto’’ alisema.
Mjumbe wa serikali ya mtaa
huo Monica Mtega alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo alimtaarifu
mwenyekiti wa mtaa ambaye hata hivyo alifika eneo la tukio na kutoa taarifa
kituo kidogo cha polisi Meta.
Kwa upande wake mwenyekiti
wa mtaa huo Elieza Ntindi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema
kuwa ameshtusha na tukio hilo kwa kuwa ni la kwanza kutokea mtaani kwake.
Alisema kuwa baada ya kupata
habari hizo alitoa taarifa polisi huku akibainisha kuwa mpaka sasa mke wa
mmiliki wa choo hicho anamuhisi mfanyakazi wake ambaye alikuwa akimchotea maji ya
kujengea nyumba ambapo inadaiwa kuwa siku chache kabla ya tukio hilo alipelekwa
hospitali baada ya kutokwa damu sehemu za siri ambaye hata hivyo anashikiliwa
na polisi kwa mahojiano.
Kutokana na tukio hilo
Ntindi, aliwaasa wasichana na wanawake kwa ujumla kuacha tabia hiyo ya kuwatupa
watoto kwani ni dhambi kwa mwenyezi Mungu na Kinyume cha sheria za nchi
Na Samwel Ndoni Mbeya, picha na Greavox Charles
|
0 comments:
Post a Comment