Friday 23 October 2015

KOCHA MAJIMAJI AMZUIYA DAKITARI KUMTIBU MCHEZAJI UWANJANI


Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Kocha Mkuu wa Majimaji FC ya Songea, Mika Lonnstrom, alimzuia daktari wa timu hiyo, Shabani Mboto kwenda kumtibu mchezaji David Burhan aliyekuwa amepata tatizo uwanjani na badala yake kuwahamasisha wachezaji wenzake wamuamshe.


Tukio hilo lilitokea juzi Jumatano wakati Majimaji ilipocheza na Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo alimkataza daktari wa timu kwenda kumtibu mchezaji huyo na kudai kufanya hivyo ni kupoteza muda wakati timu imeshafungwa, hivyo kilichokuwa kinahitajika ilikuwa ni timu kusawazisha mabao.


Mashabiki walioshuhudia tukio hilo walilifananisha na lile la Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho na aliyekuwa daktari wa timu hiyo, Eva Carneiro ambaye alimuondoa kazini kutokana na kuingia uwanjani kumtibu Eden Hazard.

0 comments: