Sunday 25 October 2015

YANAYOJIRI UCHAGUZI MKUU TANZANIA MWANZA ,DODOMA, ZANZIBAR NA GEITA

 Taaarifa hii kwa msaada bbc swahili

 4.00pm:Huko Dodoma: Katika kituo cha Majengoweyo,watu wengi wamepiga foleni huku usalama ukiimarishwa.Wapiga kura waliohojiwa wamesema wamepiga kura bila tatizo.Mwandishi wa radio free
Image captionWatangazaji wa BBC Dinah Gahamanyi na John Solombi
12.45pm:MATANGAZO MAALUM YA BBCSWAHILI YANAKUJIA KUANZIA SAA SABA KAMILI HADI SAA NANE KAMILI.PIA UNAWEZA KUTUPATA KUPITIA REDIO WASHIRIKA CLASSIC NA KISS FM
Image captionWapigaji kura wa eneo la Meko Mwanza
12.30:Katika kituo cha Meko, nje kidogo ya mji wa Mwanza, kumetokea sokomoko, baadhi ya wakazi wanalalamika kwamba majina yao hayaonekani kwenye daftari la wapiga kura.
Image captionSeif Sharif Hamad
11.30am:Mgombea wa Urais kupitia chama cha upinzani CUF, Seif Sharif Hamad amepiga kura katika kisiwa kilichopo kisiwani Unguja.
Image captionMadereva waliokosa fursa ya kupiga kura
Image captionWapiga kura waliolazimika kusafri hadi maeneo ya bara
11.00am:Baadhi ya wapiga kura waliojisajili katika maeneo mengine ya bara wamelazimika kusafiri hadi maeneo hayo ili kupiga kura.Madereva ambao hawakupewa siku ya mapumziko hawafurahii kwamba wasingeweza kushiriki katika shughuli hiyo.
Image captionJohn Pombe Magufuli
10.37am:Mgombea wa Urais kupitia chama cha CCM John Pombe Magufuli amepiga kura katika mkoa wa Kagera huko Chato
Ametoa wito kwa raia wa Tanzania kujitokeza kwa wingi ili kuwachagua viongozi wanaowahitaji.Aidha amewataka raia hao kumtanguliza mungu na kuweka amani.
Anasema kuwa alipopiga kura mvua ilianza kunyesha akisema kuwa ni ishara ya baraka.
Image captionIvory Coast
10.15am:Taifa la Ivory Coast linashiriki katika uchaguzi mkuu ulio na ushindani mkubwa ,ikiwa ni wa kwanza kabisa tangu kuisha kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011.Uchaguzi huo umeathirika baada ya wagombea maarufu wa chama cha Upinzani kujiondoa wakidai udanganyifu.
Image captionLowassa
10.00am:Mgombea wa Urais wa chama cha UKAWA Edward Lowassa ameandamana na mkewe katika kituo cha Arusha na kupiga kura
Image captionWanahakiki majina kabla ya kupiga kura
9.39am:Wakaazi wa Unguja, visiwani Zanzibar, wakihakiki majina, kabla ya kupiga kura.
Image captionDokta Shein
9.36am:Mgombea wa Rais wa CCM, Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein, akiwa katika chumba cha kupiga kura, kusini Unguja.Shein amewataka raia kujitokza kwa wingi ili kushiriki katika shughuli hiyo ya kihistoria.
Image captionMilolongo mirefu yashuhudiwa
8.36am:Takriban wapiga kura milioni 22,750,789 wanashiriki katika shughuli hiyo.
Image captionMahame
7.50am:Huku shughuli ya upigaji kura ikiendelea maeneo mengi yamesalia kuwa mahame zikiwemo barabara na maeneo mengi ya mji wa Dar es Salaam.Hii ni kwa sababu raia wengi wanashiriki katika shughuli hiyo.

0 comments: