Sunday 25 October 2015

Dakika za mwisho za CCM na UKAWA jukwaani, mzigo umepigwa Mwanza na Dar es Salaam.. (Pichaz)

October 24 2015 zimebaki saa chache mpaka sasa kuifikia October 25 siku ya Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, ni Uchaguzi ambao huwa unafanyika kila baada ya miaka kipindi mitano.
Kampeni zimefungwa rasmi leo, October 24 2015 katika Viwanja mbalimbali, nimefanikiwa kupata ripoti toka Viwanja viwili tofauti ambapo Mgombea Urais wa CHADEMA ambaye anawakilisha pia Umoja wa Vyama vya UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa alikuwa kwenye Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam, wakati huohuo Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Joseph Magufuli alikuwa Mwanza, katika Uwanja wa CCM Kirumba.
HAPA NAANZA NA MZIGO WA JUKWAA LA UKAWA, JANGWANI DAR
Hizi hapa pichaz za UKAWA Jangwani Dar pamoja na nukuu ya baadhi ya maneno yaEdward Lowassa akifunga Kampeni.
Screen Shot 2015-10-24 at 5.52.51 PM
Screen Shot 2015-10-24 at 5.52.57 PM
Screen Shot 2015-10-24 at 5.53.08 PM
Screen Shot 2015-10-24 at 5.53.15 PM
Screen Shot 2015-10-24 at 5.53.21 PM
Screen Shot 2015-10-24 at 5.53.28 PM
Screen Shot 2015-10-24 at 5.53.34 PM
Mgombea Urais anayewakilisha Umoja wa UKAWAEdward Ngoyai Lowassa.
Tuna kila sababu ya kukubaliana na Mzee Kingunge kwamba CCM imeishiwa pumzi, haina uwezo kutufikisha kwenye kilele cha mafanikio… Tunapaswa kumuelewa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alisema Chama kimoja kikikaa madarakani kwa muda mrefu kinajisahau.”>>> Edward Ngoyai Lowassa.
Screen Shot 2015-10-24 at 5.53.40 PM
Urais sio dhamana ya kutisha watu, ni wajibu wa kuongoza dira ya Taifa, anayeomba Urais anapaswa kuwa mtu aliyejiandaa… Watanzania tukubali mabadiliko.” >>> Edward Lowassa.
Screen Shot 2015-10-24 at 5.53.48 PM
Mzee Kingunge Ngombale–Mwiru akiwa kwenye Jukwaa la Funga Kampeni ya UKAWA, Jangwani, Dar Es Salaam.
Screen Shot 2015-10-24 at 5.53.53 PM
Screen Shot 2015-10-24 at 5.54.04 PM
Mgombea Urais wa Zanzibar anayewakilisha Umoja wa Vyama vya UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad.
Screen Shot 2015-10-24 at 5.54.09 PM
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima.
Screen Shot 2015-10-24 at 5.54.15 PM
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Vyama vya UKAWA, Juma Haji Duni.
Screen Shot 2015-10-24 at 5.54.20 PM
Kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Screen Shot 2015-10-24 at 5.54.27 PM
James Mbatia.
Screen Shot 2015-10-24 at 5.54.33 PM
Watu wa Huduma ya Kwanza walikuwepo pia kwa ajili ya kusaidia watu waliopata matatizo ikiwemo waliopoteza fahamu kama huyu aliyebebwa.
HAPA NAMALIZIA NA MZIGO WA CCM, UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA.
Baada ya hapo nakusogezea na hizi kutoka Uwanja wa CCM Kirumba katikati ya Jiji la Mwanza… Dk. Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan wamesindikizwa na Viongozi pamoja na wanachama wa CCM kufunga Kampeni za Uchaguzi Mkuu leoleo.
6
Rais JK akiwasili Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
3
Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli akiwasili Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
11
Rais JK alipata nafasi ya kuongelea mambo machache pia wakati wa kufungwa kwa Kampeni hizo.
Mtu kuhama CCM ni Chaguo lake, hatutohangaika kumuomba arudi… tuliopo tunatosha“– Rais Kikwete.
Haya ndio majibu ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu ishu ya RICHMOND >>> “KwenyeRICHMOND tulikubaliana kwa pamoja kwamba kwa sababu Mabwawa yetu yamekauka, tukodishe Mitambo nje ya kuzalisha Umeme, mimi sikuhusika Kampuni gani ilete Mitambo… Tatizo kwenye RICHMOND Kanuni hazikuzingatiwa
Badala ya shughuli ile kufanywa na TANESCo, Waziri Mkuu aliunda Kamati yake ya Makatibu Wakuu ifanye hiyo kazi na kutoa taarifa kwake, ndio maana Tume ya Bunge ilimwambia yeye ndio Chanzo.. ndio maana siku moja nikamwambia Tundu Lissukwamba mwenye RICHMOND yuko nae yeye.” >>> Rais Jakaya Kikwete.
IMG_9291
Waziri Msabaha aliwahi kuja akaniambia Wizara ya Fedha hawataki kutoa malipo ya kwanza kwenye hiyo Kampuni, mimi nikamwambia nawaunga mkono watu wa Wizara ya Fedha.. na nilimwambia Waziri Msabaha kuwa hiyo ni Kampuni hewa.” >>> Rais Jakaya Kikwete.
IMG_9456
IMG_9497
Rais JK na Dk. Magufuli wakiwa wameongozana na baadhi ya Wanachama wa CCM kwenye jukwaa la CCM Mwanza.

IMG_9289
IMG_9319
8
Mama Samia Suluhu Hassan na Mzee Abdallah Bulembo.

0 comments: