Monday 20 May 2013

WALIOKAMATWA VURUGU ZA MACHINGA IRINGA WAFIKA 51


WALIOKAMATWA VURUGU ZA MACHINGA NA POLISI IRINGA WAFIKIA 51 , POLISI WAJIPANGA KWA ULINZI MKALI LEO MAHAKAMANI MBUNGE PIA KUUNGANISHWA




Jeshi la  polisi  mkoa wa Iringa  limejipanga kwa ulinzi makali  leo  jumatatu  wakati  wa kufikishwa mahakamani  watuhumiwa  wa  vurugu  za umachinga mjini Iringa pamoja na mbunge  wa  jimbo  la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa .

Mbali ya  polisi  kujipanga kwa  ulinzi  pia inadaiwa  waliokamatwa mbali ya mbunge  Msigwa  ni  watu zaidi ya 51 ambapo  badhi yao  wamehojiwa na  kuachiwa  huru huku  zipo taarifa kuwa askari  wengi  zaidi  wametoka  mkoa  wa Mbeya kwa ajili ya kuweka ulinzi  zaidi katika mahakama  wakati  wa kufikishwa mahakamani mbunge Msigwa na  washirika  wake katika   vurugu  hizo.

Mtamdao  mbeyagreennews.blogspot.com umeshuhudia ulinzi makali katika kituo cha  polisi ambapo askari  wa FFU  wamezunguka  kituo  hicho huku  ndugu na jamaa wakipigwa  stop  kufika kituoni hapo kama njia ya  kuimarisha  ulinzi na usalama  zaidi.

0 comments: