Wednesday 15 May 2013

WANANCHI TARAFA YA ISIMANI WAMPONGEZA MBUNGE LUKUVI KWA UMEME NA BARABARA YA LAMI

WANANCHI TARAFA YA ISIMANI WAMPONGEZA MBUNGE LUKUVI KWA UMEME NA BARABARA YA LAMI

 

Tanesco wakiendelea  kusambaza  umeme  Tarafa ya  Isimani  jimboni kwa waziri Lukuvi
 
...................................................................................................
 
WANANCHI  wa  tarafa  ya  Isimani jimbo la Isimani  wilaya ya  Iringa  vijijini  mkoani  Iringa  wamempongeza  mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw. Wiliam Lukuvi kwa  kuwapigania kupata  umeme  wa gridi ya  Taifa  na ujenzi  wa barabara  ya lami  ya Iringa- Dodoma.

Wananchi hao  wametoa  pongezi  hizo   leo katika  ukumbi  wa Hima  wakati  wa  semina ya  siku  moja ya mradi  mpya  wa  kuwasaidia kuwakopesha  n'gombe  kupitia mradi  wa  kopa ng'ombe  lipa ng'ombe  mradi unaofadhiliwa  na asasi  ya  Heifer (HPI) 

Kwani  wamesema  kuwa  mbali ya  tarafa  hiyo ya  Isimani na  wilaya  nzima ya  Iringa vijijini katika  Historia ndio  ilikuwa ni  wilaya  pekee  iliyoweza  kulisha  mkoa wa Iringa kutokana na kuongoza katika uzalishaji  wa mazao  ya chakula  ila kwa  sasa uzalishaji huo  umebaki  kuwa  historia  baada ya  eneo hilo  kuathiriwa  zaidi na mabadiliko tabia nchi .

Hivyo   walisema maisha yao  kwa  sasa  wamekuwa  wakitegemea  jitihada mbali mbali ambazo  zimeendelea  kufanywa na mbunge  wao  huyo kutokana na kuendelea  kuwapigania  kwa  kuanzishwa kwa miradi mbali mbali  ukiwemo mradi mkubwa wa umeme ,barabara  ya lami na  sasa  mradi  wa maji ambao utatatua kero ya maji katika tarafa  hiyo ya Isimani.

Wananchi hao  walisema  kuwa  moja kati ya  changamoto  kubwa  zinazowakumba ni  pamoja na  kukosekana kwa huduma ya maji  katika  eneo  hilo kutokana na ukame  unaokabili  eneo  hilo ila kwa  sasa  suala  hilo  limekuwa  likishughulikiwa na  mbunge  wao Lukuvi. 

Bw Felix Sanga  alisema  kuwa Kuhusu tatizo la ukame  unaoendelea  kuwakumba katika tarafa    kuwa  suala  hilo  lina ufumbuzi  wake  ikiwa ni pamoja na  kujipanga kwa  utunzaji  wa mazingira  kwa  wao  wenyewe  kuweka utaratibu  wa  kutunza mazingira yanayowazunguka. 

Kuhusu  ujenzi  wa  barabara  ya lami kati ya Iringa- Dodoma  unaoendelea  Sanga alisema  kuwa  mradi huo  wa barabara  utaweza  kufungua mirango ya  kiuchumi kwa  wananchi  wa tarafa  hiyo ya Isimani na  kupongeza jitihada za mbunge na jinsi anavyoendelea  kupigania maendeleo ya  wananchi wake. 
 
 Kwa  upande  wake  mtaalam  kutoka  asasi  hiyo ya  Kimataifa ya Heifer   Interinational  Dr Emmanuel Sokonde  alisema   kuwa lengo la mafunzo  hayo ni maandalizi ya  kuandika andika  maalum kwa ajili ya  kushawishi asasi  hiyo  kusaidia miradi ya  kiuchumi  ukiwemo mradi  wa ufugaji  wa ng'ombe. 

Hivyo  alisema  kuwa  lengo la  asasi hiyo ni kuwakomboa  watanzania  na kuwatafutia miradi yenye  kuwakwamua  kiuchumi  zaidi na  kuwa iwapo  watafanikiwa  mradi huo  kufika  eneo hilo basi itakuwa ni faida kwa  wananchi wa tarafa  hiyo.

0 comments: