Saturday 25 May 2013

RAIS KIKWETE ANGIA ADDIS ABABA KWA MAAZIMISHO MIAKA 50 AU

 
 
Viongozi wa bara Afrika wanasherehekea miaka 50 tangu kuundwa na kuanzishwa kwa ulioitwa wakati huo Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) na sasa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethopia.

Mfalme Haille Selassie wa Ethiopia na wakuu wengine 31 wa nchi na serikali mbalimbali za bara la Afrika walikutana mjini Addis Ababa kuizindua OAU tarehe 25 Mei 1963 kwa majukumu la kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni ili  kufanikisha ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, hatimaye kuleta muungano wa bara lote la Afrika.

Licha ya migogoro kadhaa katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita bara la Afrika ni sehemu inayostawi haraka  kiuchumi kwa sasa.

Mwenyekiti wa Umoja huo Waziri Mkuu wa Ethopia Hailemariam Desalegn katika hotuba ya ufunguzi, amesema sherehe hizo zitatafuta kuwepo kwa bara lisilokuwa na umaskini na mizozo na Afrika ambayo raia wake wanafurahia hadhi ya kipato cha kadri.

Umoja wa Afrika (AU)  wa nchi wanachama 54 ulichukua nafasi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) uliyoanzishwa mwaka 1963  katika harakati za mataifa mengi kujinyakulia uhuru.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon, Rais wa Brazil Dilma Rouseff na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry ni miongoni mwa viongozi wa kimataifa waliojumuika na viongozi wa Afrika sherehe hizo.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande na makamu Waziri Mkuu wa China Wang Yang pia wanatarajiwa kuhudhuria.

Makundi mbali mbali ya densi yatawatumbuiza wageni waalikwa wapatao 10,000 katika mji huo mkuu wa Ethopia.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete waliwasili  jijini Addis Ababa, Ethiopia, usiku wa jana Ijumaa Mei 24, 2013 na kuungana na viongozi hao na wengine katika maadhimisho hayo.

Viongozi hao pia watakuwa na mkutano wa kawaida wa pamoja wa Umoja huo.

Zifuatazo ni picha kutoka Ikulu ya Tanzania, za matukio hayo.

 

0 comments: