Monday 20 May 2013

MAZISHI YA CHINUA CHEBE YA ANZA

MAZISHI YA CHINUA CHEBE YA ANZA   BBC Swahili -- Mazishi ya mwandishi maarufu wa riwaya wa Nigeria, Chinua Achebe, yameanza katika mji wa Ogidi, kusini-mashariki mwa nchi ambako ndiko alikotoka.

Mazishi hayo yanaendelea kwa juma zima kwa kumkumbuka na kusherehekea maisha ya mmoja kati ya waandishi maarufu kabisa wa Afrika.

Kongamano la waandishi, mihadhara ya wasomi na kanivali ni baadhi ya matukio katika mazishi ya wiki moja ya mwandishi Chinua Achebe. Shughuli zitakuwa nyingi katika mji wa Ogidi alikozaliwa kusini-mashariki mwa Nigeria. Wageni kutoka pembe zote za dunia wanatarajiwa kutoa heshima zao za mwisho kwa yule waliyemwita baba wa fasihi ya kisasa ya Afrika.

Bwana Achebe aliwakosoa viongozi wa Nigeria, lakini pamona na hayo, wanasiasa wengi maarufu wanatarajiwa kuhudhuria matanga yake.

Bwana Achebe alifariki mwezi March akiwa na umri wa miaka 82. Maziko yake yatafuata taratibu za Kikristo na utamaduni wa kabila lake la Igbo.

Chinua Achebe alikuwa maarufu kwa mtindo wake wa uandishi ambao umefuata mila ya kutoa hadithi ya kabila lake la Igbo. Kitabu chake maarufu cha “Things Fall Apart” kimetafsiriwa katika lugha zaidi ya 50 na kimetumika katika mshule ya nchi mbalimbali, ikwemo Tanzania, kwa kufundishia fasihi na lugha ya Kiingereza.


Source: BBC Swahili 

0 comments: