Saturday 25 May 2013

WANAO DAIWA KUTUHUMIWA KURUSHA BOM KANISA LAMTAKATIFU JOSEPH ARUSHA WACHIWA KWA DHAMANA


    • ARUSHA (Nipashe): Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewaachia kwa dhamana watuhumiwa wanaodaiwa kurusha bomu kwa waumini waliokuwa wamekusanyika kuanza ibada ya uzinduzi wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Mei 5, mwaka huu, jijini Arusha. Watuhumiwa hao wamepewa sharti la kuripoti polisi, pindi watakapohitajika kufanya hivyo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema: “Tumeamua kuwaachia sababu sheria haituruhusu kuendelea kuwashikilia muda mrefu na lengo letu hasa katika hili tukio hatutaki kumwonea mtu yeyote, ndiyo sababu tunafanya uchunguzi wa kina.” alisema. Hadi sasa hakuna ongezeko la mtu mwingine aliyefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo zaidi ya Victor Ambrose Kalist (20), aliyefikishwa mahakamani Mei 13 mwaka huu, mbele ya Kaimu Hakimu Mwandamizi Mkazi wa Arusha, Devotha Kamuzora, kujibu mashtaka mawili ya kuua na kujaribu kuua na kesi yake itatajwa tena Mei 27, mwaka huu; Jassin Mbarak (29), Joseph Lomayani (18), George Batholomeo Silayo (23) na Mohamed Suleiman Said (38).  HABARI KUTOKA GAZETI LA NIPASHE  JANA

    0 comments: