Saturday 18 May 2013

HALI YA MTWARA JANA HUDUMA ZA SIMAMA

 -- Hatimaye  Jana tarehe 17/05/2013 siku ambayo serikali ilikuwa iwasilishe bajeti ya Wizara ya Nishati na Madili sorry Madini lakini ikaghairi kutokana na shinikizo la WanaMtwara.   Jana Maduka karibia yote pamoja na baadhi ya ofisi zimefungwa na huduma zote zimesimama. Hali ni  ya utulivu maeneo mengi na doria ya maaskari inafanywa. Hii ni hatua muhimu sana kwa wananchi kuweza kushikamana sio kwa kudai haki pekee bali mshikamano uonekane pia katika maendeleo. UMOJA NI NGUVU!


  Hali ya usalama ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ni tete.

Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi. Usafiri wa pikipiki unapatikana katika baadhi ya maeneo machache ya mji, huku maneo makuu ya biashara yakiwa wazi bila ya pilikapilika za watu kama ilivyo kawaida.

Polisi wakiwa kwenye magari huku wakibeba silaha wameonekana katika maeneo mbalimbali ya mji, na wengine kuweka makambi madogo katika maneo yanayoaminika kuwa na msongamano wa watu katika siku za kawaida.

KUSINI imeshuhudia magari ya polisi yakiwa na askari katika maeneo ya Bima, Soko kuu ambako pia kulikuwa na 


gari la maji kumwaga maji ya kuwasha, Magomeni, Skoya na Majengo.
Hata hivyo hadi kufikia saa 7 mchana hakukuwa na hali yeyote ya uvunjifu wa amani, makundi ya vijana walionekana wakijadiliana mambo katika maeneo mengi ya mji.

Hali hiyo imejitokeza kufuatia kusambazwa kwa vipeperushi na ujumbe wa simu za mkononi na watu wasiojulikana ukiwataka wafanyabishara kusimamisha shughuli za biashara kwa siku ya   jana ili kutoa fursa kwa wananchi hao kusikiliza bajeti ya Nishati na Madini iliyotarajiwa kuwasilishwa  jana Bungeni mjini Dodoma, hata hivyo bajeti hiyo itawaslishwa Bungeni Mei, 22, mwaka huu.

Sehemu ya kipeperushi hicho kilichopambwa na picha ya motto aliyeshikia kombora kinasomeka “Wote kwa pamoja siku ya tarehe17.05.2013 (Ijumaa saa 3 asubuhi) tusikilize bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini (Bungeni) ili kujua mustakabali mzima wa gesi yetu na ili kuonyesha kilio, msimamo wetu kwa serikali wa kutaka maendeleo kwa mikoa ya kusini, siku hiyo huduma zote za jamii zisimamishwe

Licha ya polisi mkoani hapa kuwasihi wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa jeshi hilo litaimarisha ulinzi bado wananchi wameonesha kutokubaliana na wito huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa ameliambia Mwananchi kuwa hali ni shwari na kwamba jeshi lake limeimarisha ulinzi.

“Hali ni shwari, wapo madereva Bodaboda wanaendelea na kazi zao, wananchi wanatembea kama kawaida, ispokuwa baada ya maduka yamefungwa” alisema Sinzumwa.

Mwisho.


0 comments: