Saturday 25 May 2013

TFF : FIFA ITAKUWA TIBA SAHIHI KWA VIONGOZI WAROPOKAJI

TFF NA PANGA LA WAROPOKAJI



http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2013/03/Angetile-Osiah2.jpgSHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo iliyo katika mchakato wa kuundwa kwa agizo la Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), itakuwa tiba sahihi kwa viongozi waropokaji na wasio waadilifu.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya TFF jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Angetile Osiah, alisema zama za waropokaji miongoni mwa viongozi wa soka la Tanzania zinakaribia kwisha na kwamba cha moto kinakuja.
Alisema kuwa viongozi wa klabu nchini, hasa za Ligi Kuu, wamekuwa na kasumba ya kukwepa majukumu yao na kulitupia mzigo shirikisho, ambalo linapofuata sheria na kanuni, huonekana kama linafanya kazi kwa ukandamizaji.
Osiah alitoa kauli hiyo wakati akilitolea ufafanuzi sakata la usajili tata wa Mrisho Ngasa, aliyetua Yanga akitokea Simba, ambayo inadai ina mkataba naye wa mwaka mmoja anaopaswa kuutumikia baada ya kumaliza ule wa mkopo akitokea Azam FC.
“Kanuni za usajili zipo na wote mnazo na mnazitambua. Katika hili la Ngasa mnapaswa kurejea kuzisoma ili kujua zinasemaje, sio baadhi ya viongozi kuwaelekeza kwetu wakati kimsingi ni kama hatuhusiki katika mfumo wa sasa wa usajili,” alisema.
Aliongeza kuwa TFF inaamini viongozi wa klabu waliomba kazi hizo na kuchaguliwa, kwa kuaminiwa watawajibika na hawapaswi kukwepa majukumu yaliyowaweka madarakani kwa kuyakimbizia katika shirikisho.
Aidha, aliziasa klabu nchini, kujenga utamaduni wa kuwaacha makocha kufanya usajili wa wachezaji, ili kuwawezesha kuimarisha vikosi kutokana na upungufu waliouona kikosini, sio viongozi wanaosajili kwa faida binafsi.

0 comments: