Monday 20 May 2013

BUNGE LASITISHWA KWA MDA DODOMA KISA KAULI ALIYOITOA JOSEPH MBILINYI (MB MBEYA MJINI)

   

Muda mfupi uliopita spika wa bunge, Anna Makinda amelazimika kusitisha shughuli za bunge mwanzoni tu mwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikisomwa na waziri kivuli wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi aka Sugu.
waziri kivili wa whvum Joseph Mbilinyi akiwasilisha hptuba ya makadirio-Kambi rasmi ya upinzani
Kauli kwenye hotuba hiyo iliyobabisha spika wa bunge asitishe shughuli za leo hadi jioni ilisema, “Tanzania imegeuka chini ya usimamizi wa wizara ya serikali hii ya CCM kuwa taifa linalotoka nyara wanahabari, kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua.”
Spika amesitisha bunge hilo ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo kuondoa kauli za uchochezi.

0 comments: