Saturday 25 May 2013

RAIS MUSEVEN AMBADILSHA KAZI MKUU WA JESHI (UGANDA)


 
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemfuta kazi aliyekuwa Mkuu wa Jeshi nchini humo, Aronda Nyakairima na kumpa nafasi ya uraia kama Waziri wa Mambo ya Ndani.

Nyakairima alikuwa kati ya waliotajwa katika barua iliyochapishwa katika gazeti la Daily Monitor mapema mwezi huu kuhusu kuwepo njama ya kunyamazisha uvumi ulioenea kuwa Rais Museveni anataka mwanaye achukue madaraka baada yake. 

Ilidaiwa kuwa watu waliokuwa wakipinga mpango huo wangeuawa. Barua hiyo ilitoka kwa Jenerali David Sejusa mkuu wa kitengo cha usalama jeshini ambaye zamani alikuwa mpambe wa karibu wa Museveni na ambaye alitaka uchunguzi ufanyika kuhusu 'njama za kuwaua wanaopinga mpango wa kumrithi Museveni. 


Imedaiwa kuwa Nyakairima, ambaye amekuwa mkuu wa jeshi tokea mwaka 2003, alikuwa kati ya waliopangwa kuuawa. Kumekuwepo na tetesi kuwa Museveni, ambaye amekuwa madarakani tokea mwaka 1986, anataka mwanaye wa kiume, Brigedia Kainerugaba Muhoozi achukue urais pale muhula wake utakapomalizika mwaka 2016.  


Serikali ya Uganda imefunga vyombo kadhaa vya habari ikiwa ni pamoja na gazeti la Daily Monitor kwa kuchapisha barua hiyo ambayo imetajwa kuwa ya kichochezi. 


Katika taarifa siku ya Ijumaa, Jeshi la Uganda limesema Nafasi ya Nyakairima imechukuliwa na Luteni Jenerali Katumba Wamala. Museveni pia amefanya mabadiliko kadhaa katika baraza la mawaziri na makatibu wa wizara.



Source:  via Radio Tehran, IRAN

0 comments: