Friday 17 May 2013

MLINZI ACHINJWA MOROGORO

PictureHabari na DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO 

---

MLINZI wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam jirani na daraja la Mzambarauni, Bw Mika Athumani amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.

Mmiliki wa bar hiyo Bw Salvatory Mushi alidai inaonekana kwamba majambazi hao walimvamia mlinzi wake na kumchinja na baadaye walivunja "counter" ya baa hiyo pamoja na duka ililipoj irani nakuiba vitu mbalimbali.

Mushi anasema bado hajafahamu thamani ya vitu vilivyoibwao.

Baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo la tukio walidai kwamba mlinzi huyo alikuwa amelala hivyo majambazi hayo yalimvamia na kumpora silaha zake kirahisi kabla ya kumchinja," siumeona alikuwa amelala jirani na baiskeli yake ndio maana ameshindwa kupamabna nao... ukizingatia baa hii imejitenga iko peke yake hapa jirani na mto,"alisema Bw Maneo Mashani.

0 comments: