Saturday 18 May 2013

KAVUMBAGU NA HAMISI KIZA WAILIZA SIMBA LEO

  SIMBA  ABANWA NA YANGA  MBAVU LEO KTK UWANJA WA TAIFA

 MABINGWA YANGA 2 SIMBA 0


 Picture Picture
MABINGWA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Yanga, leoYANGAwamemaliza Msimu wa 2012/13 kwa furaha kubwa baada ya kuwatandika Wapinzani wao wa Jadi Simba kwa Bao 2-0 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Yanga, ambao waliutwaa Ubingwa mapema wakiwa na Mechi kadhaa mkononi, walianza Mechi hii kwa kishindo na Didier Kavumbagu ndie alieanza sherehe za kupokea Kombe la Ubingwa mapema alipofunga Bao katika Dakika ya 4 tu.

YANGA-BIN_KLEIB_n_BRANDTSSimba walipata nafasi murua ya kusawazisha Bao hilo katika Dakika ya 28 walipopewa Penati kufuatia Nadir Haroub 'Cannavaro' kumuangusha Mrisho Ngassa lakini Mussa Mudde akakosa Penati hiyo.

Hadi Mapumziko Yanga 1 Simba 0.

Kipindi cha Pili, Dakika ya 63, Hamis Kiiza alifungia Yanga Bao la Pili.

Mechi hii nusura iingie hitilafu katika Dakika ya 89 baada ya Cholo wa Simba na Kavumbagu kuvaana na Refa Martin Saanya alipoingilia kati akaanguka na alipoinuka alionekana kutokwa damu lakini Mechi iliendelea.

Hii ni mara ya Pili Timu hizi kukutana Msimu huu kweye VPL na mara ya kwanza matokeo yalikuwa Bao 1-1 hapo Oktoba 3, 2012.

VIKOSI:

Yanga: Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Athuman Idd 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima

Akiba: Said Mohamed, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nurdin Bakar, Nizar Khalfan, Said Bahanuz, Jerry Tegete

Simba: Juma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, Haruna Chanongo

Akiba: Abel Dhaira, Miraji Adam, Ramadhan Singano 'Messi', Felix Sunzu, Christopher Edward, Jonas Mkude, Hassan Mkude

REFA: Martin Saanya [Morogoro]

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

RATIBA/MATOKEO:

Jumamosi Mei 18

Simba SC 0 Yanga 2

Toto Africans Vs Ruvu Shooting

Mgambo JKT Vs African Lyon

JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar

TZ Prisons Vs Kagera Sugar

JKT Oljoro Vs Azam FC

Polisi Moro Vs Coastal Union
MSIMAMO:
***YANGA+++BINGWA
NA TIMU P W D L GF GA GD PTS
1 YANGA 26 18 6 2 47 14 33 60
2 AZAM FC 25 15 6 4 45 20 25 51
3 SIMBA SC 26 12 9 5 38 25 13 45
4 KAGERA SUGAR 25 11 8 6 26 19 7 41
5 MTIBWA SUGAR 25 10 9 6 29 24 5 39
6 COASTAL UNION 25 8 11 6 25 23 2 35
7 RUVU SHOOTING 25 8 8 9 22 24 -2 32
8 JKT OLJORO 25 7 8 10 21 26 -5 29
9 TANZANIA PRISONS 25 7 8 10 16 22 -6 29
10 JKT RUVU 25 7 5 13 21 38 -17 26
11 MGAMBO SHOOTING 25 7 4 14 16 27 -11 25
12 POLISI MOROGORO 25 4 10 11 13 23 -10 22
13 TOTO AFRICAN 25 4 10 11 21 33 -12 22
14 AFRICAN LYON 25 5 4 16 16 38 -22 19

0 comments: