Wednesday 3 December 2014

ILO NA TUCTA WANDAA SEMINA YA MAFUNZO BURE JIJINI MBEYA IJUMAA HII


Mkugenzi wa wise and mercy compani Clemence Busara Akiwa ofisini kwake


Shirika la kazi duniani  ILO  na chama cha wafanyazi Tanzania TUCTA kwa kushirikiana na wise and mercy company ameandaa  Semina kubwa ya mafunzo ya kuelimisha juu ya kujua msingi ya  na sheria  za kazi kwa mwajiri na majiriwa

Akizungumza na mtandao huu wa green media ofisini kwake  Mkurungenzi wa wise and mercy company ambao ni ndiyo waratibu wa mafunzo haya Mh Clemence Busara amesema kuwa lengo kubwa la semina  hii ni kumjengea uwezo mfanyakazi  kueleawa misingi ya kazi kwa mwajiri na mwajiriwa ,kutambua wajibu wa mwajiri na mwajiriwa katika majukumu ya kila siku,  kuwongeza  ujuzi zaidi mfanyakazi  kufanya kazi kwa Ufanisi na Ubunifu wa hali ya juu.na jinsi mwajiri anavyo weza kuboresha mazingira kwa wafanya kazi wake.
Mkugenzi wa wise and mercy compani Clemence Busara Akiongea na mwandishi wa Habari wa Green Media Group {Abdul Marwa Abdallah} 
Mh busara ameongaza kuwa ILO na TUCTCA wameona kuna umuhimu mkubwa wa kuandaa mafunzo haya kwa kuwa wanyakazi wengi hawatambui sheria za kazi zinazo walinda wakiwa kwenye ajirazao, wajiri kukiuka miko  na sheria za kazi kwa wajiriwa, busara amesema kupitia mafunzo haya  yanaweza kuondoa hali ilipo hivi sasa
 Mkugenzi huyu amesema mafunzo haya yamewalenga   Wajasiriamali Wadogo na wakubwa, wafakazi wa umma nawa mashrika binafsi ,wakurungenzi wa kampuni na tasisi mbalimbali, hivyo ametoa wito kwa watu wote kuhudhuria kwa  kwa wingi kwa kuwa mafunzo hayo kwa kuwa semina hiyo ni bure
Mafunzo hayo yatafanyika   nyanda ya juu kusini mkoa wa mbeya Siku ya Ijumaa 5/12/2014  katika ukumbi wa JM MOTEL, karibu na shule ya st merry kuanzia 10:00 kamili asubuhi  na  kingilio cha mafunzo haya ni bure kwa mtu yeyote Yule ,semina ya mafunzo hayo itahudhuliwa na wa wawakilishi wa sirika la kazi duiani (ILO) ,chama cha wafanya kazi Tanzania TUCTA , wawakilishi wa wizara ya kazi  mkoa wa mbeya  na wadau mbalimbali  hapa nchini Tanzania.
clemence busara akiwa ofisini kwake
Ikumbuke kwa semina hii ya mafunzo inaratibiwa na kusimamiwa na wise and mercy company kwa kuwezeshwa na ILO na TUCTA kushirikiana  wizara ya kazi mkoa.

0 comments: