Monday 15 December 2014

Zaidi ya watu 129 wazama Ziwa Tanganyika DR Congo


Maboti katika eneo hilo mara nyingi hujazaa abiria na mizigo kupita kiasi na ajali kutokea ni jambo la kawaida

Miili ya watu 129 imepatikana katika Ziwa Tanganyika baada ya boti kuzama Ijumaa

Miili ya watu wapatao 129 imepatikana kutoka Ziwa Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya feri kupinduka na kuzama mapema Ijumaa.
Waziri wa Uchukuzi nchini humo Laurent Sumba Kahozi amesema msako unaendelea kuwatafuta watu waliopotea katika ajali hiyo.
Wafanyakazi wa uokoaji waliwapata abiria wakielea katika maji Jumapili, wakiwa katika mapipa ya petroli na vifaa vingine.
Habari zinasema ajali kama hiyo ni za kawaida katika eneo hilo kutokana na boti kujaa abiria na mzigo kupita kiasi.
Maboya ya kujiokoa mara nyingi hayamo katika maboti hayo na watu wengi hawawezi kuogelea.
Maafisa katika jimbo la Katanga wamesema upepo mkali na kujaza abiria na mizigo kupita kiasi kumesababisha boti MV Mutambala, kupinduka.
Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Wanawake na watoto ni miongoni mwa watu waliokumbwa na ajali hiyo ambayo ilitokea mapema Ijumaa asubuhi.
Taarifa za awali zilisema watu 26 wamekufa katika ajali hiyo.
Idadi ya watu walionusurika imetajwa kuwa watu 232, wengi wakiwa ni wanaume, amesema waziri wa uchukuzi katika eneo hilo

0 comments: