Monday 15 December 2014

ENRIQUE ASISITIZA LICHA YA SARE, BARCELONA BADO NI BORA


Kocha Luis Enrique amesema hajakatishwa tamaa na uchezaji wa kikosi chake cha Barcelona.

Barcelona ilibanwa na kutoka sare na Getafe katika mchezo ulioonyesha kuwaudhi mashabiki wa Barcelona.
“Unajua inavyokuwa ngumu kama umeingia na sasa ndiyo tuko kwenye mabadiliko.

“Lakini ugumu unaongezeka kama haukutumia nafasi vizuri,” alisema.
“Nisisitize, kama utazungumzia ubora wa timu, basi timu yetu ni bora na sare haiwezi kutuondoa katika hilo,” alisistiza.


“Kikubwa kinachotakiwa ni kutatua matatizo yaliyotokea katika mechi hiyo, halafu tusonge mbele, hilo ndilo jambo la msingi zaidi.”

0 comments: