Monday 15 December 2014

Wachezaji wa ti mu ya Zambia wapata ajali mbaya


  •  
Maafisa wakuu wa klabu hio wanasema hali ya wachezaji waliojeruhiwa imeweza kuimarika
Wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia waliohusika katika ajali ya barabarani Jumapili, wanasemekana kuwa katika hali nzuri.
Wachezaji hao Nyambe Mulenga, ambaye huchezea klabu ya Zesco United, Changwe Kalale wa Power Dynamos na Satchmo Chakawa kutoka Green Eagles walikuwa wanakwenda mjini Lusaka kwa basi ndogo la klabu ya Zesco United.
Basi hilo liligongana ana kwa ana na gari lengine katika eneo la Kabwe.
Shirikisho la soka nchini humo lilisema watu kadhaa walijeruhiwa na kwamba Mulenga alivunjika mguu.
Duru katika eneo hilo zilisema kuwa dereva wa basi la Zesco alifariki katika eneo la ajali huku watu wangine watatu waliokuwa kwa gari la pili pia wakifariki.
Klabu hio imetoa taarifa kuhusu hali ya wachezaji waliohusika na ajali hio pamoja na maafisa wengine wa klabu waliokuwa ndani ya basi hio.
Mhasibu wa klabu hio, Lomuthunzi Mbeba, afisa wa mauzo Fusya Bowa, afisa Frank Chitambala na mwanchama wa kamati Peter Mutale pia walijeruhiwa ingawa wanasemekana kua katika hali nzuri.
Kalusha Bwalya, Rais wa shirikisho la soka Zambia, alithibitisha kuwa maafisa waliojeruhiwa walifikishwa hospitalini na kwamba hali zao zimeimarika.
Wachezaji walikua wanasafiri kuelekea mjini Lusaka kwa maandalizi ya michuano ya kombe la mataifa ya afrika 2015. Michuano hio inaanza tarehe 17 Januari nchini Equatorial Guinea.
Zambia itacheza katika kundi B pamoja na DR Congo, Cape Verde na Tunisia.

0 comments: