Wednesday 3 December 2014

WAYNE ROONEY KUPIMWA GOTI LEO, DELAY BLIND APONA!


ROONEY-LVG-KICHEKO-18OCTWAKATI Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney Leo hii atapimwa Goti lake kuthibitisha undani wa maumivu yake na pia atakuwa nje kwa muda gani, Klabu hiyo imepata habari njema baada ya Kiungo Daley Blind kupata nafuu na huenda akawa fiti kabisa kabla ya mwisho wa Mwezi huu baada nae kuumia Goti.
Rooney hakucheza Mechi ya Ligi Kuu England Jumanne Usiku Uwanjani Old Trafford wakati Man United inaifunga Stoke City 2-1 baada kuumia Goti Jumamosi iliyopita wakati wanaifunga Hull City.
Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema: “Rooney atachunguzwa zaidi Goti lake Jumatano. Natumai hakuumia sana.”
Nae Blind alieumia Goti akiichezea Timu ya Taifa ya Netherlands anatarajiwa hivi karibuni kurejea Mazoezini.
Tangu aanze kuifundisha Man United, Van Gaal amekumbwa na Majeruhi wengi na kwenye Mechi na Stoke City Mastaa wake wakubwa kina Angel Di Maria, Luke Shaw na Daley Blind vile vile hawakucheza.

Manchester United-Listi ya Wachezaji walioumia Msimu huu:
Kipa: David De Gea
Viungo: Angel Di Maria, Juan Mata, Michael Carrick, Daley Blind, Ashley Young, Ander Herrera, Antonio Valencia, Anderson, Marouane Fellaini, Jesse Lingard
Mabeki: Rafael, Luke Shaw, Phil Jones, Marcos Rojo, Jonny Evans, Chris Smalling, Paddy McNair, Tom Thorpe
Mafowadi: Radamel Falcao, Wayne Rooney, Robin van Persie, James Wilson

Van Gaal amethibitisha kuwa Rooney na Di Maria hawataweza kucheza Mechi yao ijayo ya Ligi Jumatatu Ugenini na Southampton kwani ni mapema mno kwao.
Hata hivyo, Van Gaal amesema majeruhi wao wengi sasa wanapona na wameanza kurejea Mazoezini.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumatano Desemba 3
2245 Arsenal v Southampton               
2245 Chelsea v Tottenham         
2245 Everton v Hull         
2245 Sunderland v Man City                
Jumamosi Desemba 6
1545 Newcastle v Chelsea           
1800 Hull v West Brom               
1800 Liverpool v Sunderland                
1800 QPR v Burnley          
1800 Stoke v Arsenal       
1800 Tottenham v Crystal Palace          
2030 Man City v Everton            
Jumapili Desemba 7
1630 West Ham v Swansea                   
1900 Aston Villa v Leicester                  
Jumatatu Desemba 8
2300 Southampton v Man Utd

0 comments: