Sunday 16 March 2014

BPL MSIMU MAJANGA MAN UNITED: YAFUNGWA BAO 3-0 NA LIVERPOOL!! KADI NYEKUNDU VIDIC NJE!

>>REFA MARK CLATTENBURG AWAPA LIVERPOOL PENATI TATU, KADI NYEKUNDU VIDIC!
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Machi 16
Man United 0 Liverpool 3
[Saa za Bongo]
1900 Tottenham v Arsenal

MAN_UNITED-MOYES_A_GENIUSMSIMU WA MAJANGA kwa Manchester United umeendelea Leo Uwanjani kwao Old Trafford baada kufungwa Bao 3-0 na Mahasimu wao wakubwa Liverpool katika Mechi ya Ligi Kuu England huku Bao mbili zikifungwa kwa Penati na la Tatu kwa Bao ambalo Wachezaji wa Man United walilalamika sana ni Ofsaidi.
Refa Mark Clattenburg aliwapa Penati ya Kwanza Liverpool katika Dakika ya 34 baada ya Rafael kunawa Mpira na Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, kufunga.FERGUSON_AKISHUHUDIA_MAJANGA
Sekunde 25 tu tangu Kipindi cha Pili kuanza, Refa Mark Clattenburg aliwapa tena Liverpool Penati ya Pili kwa madai Phil Jones alimchezea Rafu Joe Allen na Steven Gerrard kufunga tena.
Na kama hizo hazikutosha, Refa Mark Clattenburg aliwapa tena Liverpool Penati ya Tatu na kumpa Kadi ya Njano ya Pili Nahodha wa Man United Nemanja Vidic, na hivyo kumtoa kwa Kadi Nyekundu, kwa madai ya kumuangusha Daniel Sturridge wakati Mchezaji huyo hakuguswa hata kidogo lakini Penati hiyo, iliyopigwa tena na Gerrard, iligonga Posti na kuokolewa.
Man United tena walipatwa na dhoruba wakati Luis Suarez, akiwa wazi Ofsaidi, kuipa Liverpool Bao la Tatu.
Mbali ya Matukio hayo, Man United mara zipatazo mbili walidai Penati kwao na Refa Mark Clattenburg kupeta.
VIKOSI:
MAN UNITED: De Gea, Da Silva, Jones, Vidic, Evra, Fellaini, Carrick, Mata, Rooney, Januzaj, Van Persie

Akiba: Ferdinand, Lindegaard, Young, Welbeck, Cleverley, Valencia, Kagawa.

LIVERPOOL: Mignolet, Johnson, Skrtel, Agger, Flanagan, Henderson, Gerrard, Allen, Sterling, Sturridge, Suárez


Akiba: Brad Jones, Aspas, Coutinho, Moses, Sakho, Cissokho, Lucas.

Refa: Mark Clattenburg

MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Chelsea 30 33 66
2 Liverpool 29 41 62
3 Man City 27 44 60
4 Arsenal 28 24 59
5 Tottenham 29 0 53
6 Man United 29 9 48
7 Everton 28 11 51
8 Newcastle 28 -2 43
9 Southampton 30 2 42
10 Aston Villa 29 -6 34
11 West Ham 28 -4 31
12 Stoke 29 -14 31
13 Hull 29 -7 30
14 Swansea 28 -4 29
15 Norwich 29 -22 29
16 Crystal Palace 28 -19 27
17 West Brom 28 -11 25
19 Cardiff 29 -28 25
18 Sunderland 26 -16 24
20 Fulham 29 -36 21
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Machi 22
1545 Chelsea V Arsenal
1800 Cardiff V Liverpool
1800 Everton V Swansea
1800 Hull V West Brom
1800 Man City V Fulham
1800 Newcastle V Crystal Palace
1800 Norwich V Sunderland
2030 West Ham V Man United
Jumapili Machi 23
1630 Tottenham V Southampton
1900 Aston Villa V Stoke
Jumanne Machi 25
2245 Arsenal V Swansea
2245 Man United V Man City
2245 Newcastle V Everton
Jumatano Machi 26
2245 West Ham V Hull
2300 Liverpool V Sunderland

0 comments: