Tuesday 17 November 2015

KAZI sasa imeanza BomoaBomoa Kubwa ya Nyumba Kuanza Leo Jijini Dar


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UBOMOAJI WA NYUMBA MANISPAA YA KINONDONI


Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
 Maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.
Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
i.                     Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini yaliyotengwa kwa shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa ili yasivamiwe.
Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
ii.                    Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika maeneo yao. 
Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hili la ubomoaji.
Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa
  a)     Bila kibali cha ujenzi
  b)     Bila kufuata michoro ya mipango miji
  c)      Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)
Zoezi hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya Ardhi itasimamia sera za ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.
Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji huu ni  Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni – Biafra. Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe 18/11/2015 hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.

0 comments: