Tuesday 17 November 2015

Makamu wa kwanza wa rais Serikali ya Maalim Seif azua balaa lingine CCM



 
Na Jabir Idrissa, Zanzibar

WAKATI wananchi hawajui hasa kinachojadiliwa kwenye vikao vya viongozi wakubwa waki wemo wastaafu Zanzibar, kuna fununu kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuna mvutano wa nani atashika wadhifa wa makamu wa kwanza wa rais wa kushiriki Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoundwa na Maalim Seif mara akishatangazwa mshindi wa uchaguzi uliokwisha.

 
Taarifa kutoka ndani ya serikali, chama hicho zimesema kwamba inaonekana jina la Balozi Seif Ali Iddi ni kama halipendezi kwa pande zote mbili? upande wa chama alicho cha CCM, na upande wa Maalim Seif ambaye yumo katika kupigania haki yake ya kuongoza Zanzibar kwa kuwa ametoa takwimu zilizothibitishwa ndani ya Tume ya Uchaguzi kuwa zimempa ushindi wa urais kufuatia kura zilizopigwa Oktoba 25, mwaka huu.

Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), amegombea wadhifa huo mara ya tano mfululizo, safari hii akiwa amefanikiwa kukusanya ushahidi wa wazi kuwa amechaguliwa na wananchi kwa zaidi ya asilimia 53.

 Gazeti hili limefahamishwa na vyanzo vyake kwamba CCM baada ya kusalimu amri kuhusu kudai kuwa kimehujumiwa lakini kikipaisha malalamiko yake kinyume na utaratibu wa kisheria, viongozi wake wanahangaika kupata mtu atakayeshika umakamu wa kwanza, ule ambao Maalim Seif amemaliza kuutumikia kwa miaka mitano hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, ambayo mabadiliko yake ya mwaka 2010, ndiyo yaliyozaa utaratibu wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ikiongozwa na Rais na kusaidiwa na makamu wawili, mmoja kutoka chama kinachoibuka cha pili katika matokeo ya uchaguzi, safari hii itahitajika CCM ndio wateue makamu wa kwanza.

Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 39(1), inasema? Kutakuwa na makamu wawili wa rais ambao watajulikana kama makamu wa kwanza wa rais na makamu wapili wa rais. Kifungu cha 3 inaelezwa, ?Makamu wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa rais.?

Kama Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambayo Mwenyekiti wake Jecha Salim Jecha, alitoa taarifa Oktoba 28 ya kufuta uchaguzi mzima, itarudi kazini na kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya kura za urais za majimbo

0 comments: