Friday 13 November 2015

MAALIM SEIF ASEMA HATASHIRIKI MARUDIO YA UCHAGUZI ZANZIBAR


Mgombea wa Chama Cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesisitiza kuwa Chama hicho hakitashiriki katika uchaguzi wa marudio kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa mwezi uliopita. Maalim Seif ameyasema hayo jijini Dar es Salaam hii leo baada ya kikao chake na viongozi wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA akiwemo aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania kupitia CHADEMA na kuungwa mkono na UKAWA Edward Lowassa.

cHANzo dw swahili

0 comments: