Wednesday 4 November 2015

Wananchi wa Dakawa wanalazimika kutumia maji yenye kinyesi cha wanyama.

 Wananchi wa kijiji cha wami Sokoine wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wamelalamikia kutumia maji machafu yanayotumiwa na mifugoa kwa muda mrefu hali inayotishia afya za wananchi hao kwa kuhofia kupata magonjwa.
Wakizungumza kwa masikitiko  wananchi hao wamesema wanalazimika kununua  maji shilingi 1,500 kila dumu la lita 20 ambapo wamesema wanashangazwa na hatua ya serikali kushindwa kufanya jitihada  za kuwapatia maji wananchi wa kijiji hicho  hali ya kuwa wanalipa kodi  kama watanzania wa maeneo mengine.
 
Aidha wananchi hao wamesema kufuatia ukosefu wa maji katika kijiji hicho wamelazimika kutumia nguvu zao kuchimbua Tope lililojaa  kwenye bwawa linalotumiwa na mifugo  ili kuongeza kina na liwe na uwezo wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu ambapo wameiomba serikali na wadau  kuwasaidia greda la kuchimbua tope ili kurahisisha kazi hiyo.
 
Akijibu malalamiko ya wananchi hao  kwa njia ya simu diwani mteule wa kata ya wami Sokoine Yusuph Athumani amesema tayari serikali imekwisha anza jitihada za kutandaza  mabomba ili kuhakikisha wananchi wa eneo hilo wanaondokana na adha ya ukosefu wa maji.


Chanzo: ITV Televition

0 comments: