Wednesday 4 November 2015

MATOKEO YAFC Bayern Munich Vs Arsenal na matokeo ya mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa Ulaya November 4


Michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya hatua ya Makundi imeendelea tena usiku wa November 4 kwa michezo nane kupigwa ikihusisha timu kutoka Kundi EFG na H, zikiwa timu zote zilizocheza usiku wa November 4 zilikuwa zinacheza mchezo wake wa nne, klabu ya FC Bayern Munich iliikaribisha Arsenal katika dimba la Allianz Arena.
3589
FC Bayern Munich wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa Arsenalmchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa nyumbani wa Arsenal Emirates, wamelipiza kisasi kwa kuifunga Arsenal jumla ya goli 5-1 na kutimiza jumla ya point 9 katika msimamo wa Kundi F huku ikiongoza kwa utofauti wa magoli 10 ya kufunga na kufungwa.
Arsenals-Francis-Coquelin-in-action-with-Bayern-Munichs-Douglas-Costa
Magoli ya FC Bayern Munich yalifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 10, Thomas Muller aliyefunga goli mbili dakika ya 29 na 89, David Alaba dakika ya 44 na Arjen Robben dakika ya 55 na Arsenal kuambulia goli moja lililofungwa na Oliver Giroud dakika ya 69, kwa matokeo hayo klabu ya Arsenal itakuwa na nafasi ndogo ya kufuzu kwenda hatua ya 16, kwani inatakiwa ishinde kwa idadi kubwa ya magoli katika mechi zake mbili zilizosalia huku ikiomba dua Olympiakos ipoteze kwa kufungwa mechi zote mbili zilizosalia.
3008
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa November 4
Kundi E
  • Barcelona 3 – 0 BATE Borisov
  • Roma 3 – 2 Bayer Leverkusen
Kundi F
  • Bayern Munich 5 – 1 Arsenal
  • Olympiakos 2 – 1 Dinamo Zagreb
Kundi G
  • Chelsea 2 – 1 Dynamo Kyiv
  • Maccabi Tel Aviv 1 – 3 FC Porto
Kundi H
  • Gent 1 – 0 Valencia
  • Lyon 0 – 2 Zenit St. Petersburg
  

0 comments: