Sunday 15 November 2015

Polisi walazimika kupiga mabomu hospitali ya Bugando kutawanya waombolezaji.


Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limelazimika kupiga mabomu ya machozi katika hospitali ya rufaa Bugando ili kumuokoa askari mwenzao aliyekuwa ameingia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, baada ya mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema ) mkoa wa Geita Alphonce Mawazo kuwasili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 11.30 jioni baada ya viongozi wa Chadema na wafuasi wao kufikisha mwili wa mawazo ambaye katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu aligombea ubunge wa jimbo la Busanda, huku askari hao waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi wakimkamata mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema taifa Patrobas Katambi kwa mahojiano zaidi.
 
Mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema amezungumzia kifo cha Alphonce Mawazo, aliyewahi kuwa diwani wa kata ya Sombetini Arusha kwa tiketi ya chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
 
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita Alphonce Mawazo aliuawa kinyama baada ya kushambuliwa kwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Geita.

0 comments: