Tuesday 29 April 2014

WANDISHI WA HABARI 9 WAKAMATWA NCHINI ETHIOPIA


 

Kamati ya kutetea haki za waandishi habari imelaani vikali kitendo cha serikali ya Ethiopia cha kuwakamata waandishi habari 9 , wakielezea kama ni hatua mbaya zaidi kuchukuliwa na serikali hiyo dhidi ya uhuru wa kujieleza nchini humo.
Mamlaka ya Addis Ababa imedai waandishi hao wa magazeti na mitandao ya kijamii wanatumia nafasi zao kujaribu kuvuruga amani nchini humo.
Waziri wa mambo ya nje wa marekani anatarajiwa kuwasili nchini humo leo kuanza ziara ya mataifa matatatu katika kanda hii ikiwemo Angola na Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo.
Watetezi wa haki za binadamu wamemhimiza kuzungumzia swala hilo.
Serikali ya Ethiopia inaendeelea kukaza kamba na kukandamiza uhuru wa kujieleza kwa watu nchini humo hali ambayo imesababisha maandamano kwa wiki mbili zilizopita
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International, kukamatwa kwa wanablogu sita wiki jana ni sehemu ya mpango wa serikali kukandamiza upinzani.

0 comments: