Sunday 27 April 2014

KOCHA MPYA WA TAIFA STARS,AMEONGEZA WACHEZAJI TISA KATIKA KIKOSI, YONDANI ATEMWA

MartNooijKocha mpya wa Taifa Stars, Mart Nooij ameongeza wachezaji tisa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi (The Flames) itakayochezwa Mei 4 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. 
Wachezaji walioongezwa ni Edward Charles Manyama (JKT Ruvu), Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam), Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa).
Naye beki Kelvin Yondani wa Yanga ambaye aliitwa awali ameondolewa katika kikosi hicho kwa vile ameshindwa kuripoti kambini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Pemium Lager inaingia kambini kesho (Aprili 28 mwaka huu) jijini Mbeya kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

0 comments: